30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi waanza uchunguzi kifo cha Balozi

Bernard Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe

Asifiwe George na Victoria Kanje (RCT), Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam limeanza uchunguzi kuhusu kifo cha Balozi wa Libya nchini, Ismail Hussein Nwairat (39) ambaye alijipiga risasi juzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova, alisema balozi huyo alifariki Julai mosi, mwaka huu saa 13:15 mchana kwa kujipiga risasi.

Balozi Nwairat alijiua kwa kujipiga risasi akiwa amejifungia ndani ya Ofisi ya Ubalozi wa Libya, uliopo Mtaa wa Mtitu, Upanga.

Kova alisema hivi sasa Jeshi hilo linafanya uchunguzi, ikiwamo kujua sababu za Balozi huyo kuamua kujiua na tayari wamepatiwa kibali cha kuanza kazi hiyo.

“Uchunguzi huo utawahusisha wataalamu wa kuchunguza vifo vya aina hii kutoka Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ubalozi wa Libya na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ili kukamilisha uchunguzi huo pamoja na hatua nyingine muhimu za tukio hili,” alisema Kova.

Kaimu Balozi Nwairat amejiua kwa kujipiga risasi ofisini kwake juzi, hadi sasa bado haijafahamika ni kwanini amechukua uamuzi huo.

Balozi Nwairat alijifungia ofisini kwake na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza linafanya uchunguzi kuhusu tukio la kushambaliwa kwa basi la Magereza namba T0046 aina ya Isuzu, lililotokea juzi Mikocheni, jijini Dar es Salaam, jirani na Regency Hotel.

Kova alisema tukio hilo lilitokea saa 13:30 mchana ambapo watu wasiofahamika walilishambulia basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Askari Magereza namba A.9716 SGT Msofe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles