29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm: Ubingwa bado sana

plujimNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema bado ni mapema sana kutabiri kuwa timu hiyo itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kufanikiwa kuwachapa watani wao wa jadi, Simba mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu, juzi waliendeleza kasi yao na kurejea kileleni kuongoza katika msimamo wa ligi huku wakiwaongezea machungu mahasimu wao kwa kutoa kipigo cha pili mfululizo msimu huu.

Yanga wanashika usukani wa ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 46 baada ya kushuka dimbani mara 19 wakifuatiwa na Azam FC waliopo nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 45 sawa na Simba wakitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumza Dar es Salaam juzi mara baada ya pambano hilo la watani wa jadi, Pluijm alisema hawezi kutabiri kuwa Yanga itakuwa bingwa kwa kuwa wamemfunga Simba wakati kuna michezo mingi inayowakabili Ligi Kuu.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, alisema aliwajua vizuri wapinzani wake ndiyo maana alijiandaa kwa kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo ili kuitibulia Simba mipango yake.

Alisema wachezaji wake walicheza kwa kiwango cha hali ya juu na kujituma uwanjani ambapo waliweza kuwakabili vilivyo mahasimu wao kwani hata ushindi waliopata haikuwa kazi rahisi kwa upande wao.

“Nilipanga kikosi kulingana na ushindani ambao tulitarajia kukutana nao ndiyo maana tuliweza kuibuka na ushindi mnono mbele ya wapinzani wetu,” alisema.

Juzi Yanga walidhihirisha kuwa wao ni wababe wa Simba kwa msimu huu baada ya kutoa kipigo cha pili mfululizo ambao awali katika mzunguko wa kwanza walifanikiwa kuwafunga mabao 2-0.

Msimu huu Yanga wamejizolea pointi sita kutoka kwa Simba tofauti na msimu uliopita ambao walitoka suluhu katika mzunguko wa kwanza kabla ya kufungwa bao 1-0 waliporudiana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles