25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wachezaji Simba wabebeshwa lawama

Mayanja-J-1NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KOCHA wa Simba Mganda, Jackson Mayanja, amewatupia lawama wachezaji wake akidai wameshindwa kufuata maelekezo aliyowapa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga uliofanyika juzi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ambao walikuwa na rekodi ya kushinda mechi mfululizo, juzi walijikuta wakitibuliwa kasi yao baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Yanga kipigo ambacho ni cha kwanza kwa Mayanja.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema wachezaji walimwangusha kwa kucheza tofauti na mambo waliyokuwa wakifundishwa kwenye mazoezi kujiandaa na pambano hilo.

“Wachezaji wameniangusha kwa sababu hawakuweza kuyafanyia kazi maelekezo niliyokuwa nikiwapa mazoezini na matokeo yake tumepoteza ushindi mbele ya mahasimu wetu,” alisema.

Alisema pamoja na kukosa ushindi ataendelea kuyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza ili yasijirudie katika michezo mingine inayowakabili kwenye ligi hiyo ambayo wamefikia raundi ya 20.

Kocha huyo ambaye ameonja kipigo cha kwanza tangu aanze kukinoa kikosi hicho, alisema atazidi kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake ili waweze kusahau yaliyopita na kuendeleza kasi ya ushindi waliyokuwa nayo na kuendelea kubaki nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

Kutokana na matokeo ya juzi, Simba imeshuka hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia pointi 45 sawa na Azam FC wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles