28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm: Chuma ‘kikoli’ moto Yanga

pluijm*Akwepa kumzungumzia Niyonzima aliyesimamishwa

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans Van Pluijm, ametamba kuwa sasa mambo yamepamba moto katika kikosi chake, baada ya kombinesheni kukubali kwenye kikosi chake ambacho juzi kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao hayo yalifungwa dakika ya 18, 39 na 45 yote yakipachikwa nyavuni na Amissi Tambwe, wakati bao la nne liliwekwa kimiani na Thaban Kamusoko dakika ya 63.

Tambwe ambaye aling’ara katika mchezo huo, aliiandikia Yanga hat-trick ya kwanza msimu huu, ikiwa ni ya tatu kwenye ligi kwani ya kwanza ilikuwa ya Hamis Kiiza na kufuatiwa na Ibrahim Ajibu wote wa Simba.

Akizungumza Dar es Salaam juzi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Pluijm alisema wachezaji wake wamemfurahisha sana kuanzia namna ya uchezaji wao hadi aina ya mabao waliyofunga, hivyo kuridhika na ushirikiano wao.

“Kombinesheni imekubali, wamecheza vizuri hata aina ya mabao yaliyofungwa yalikuwa mazuri sana, pasi walizokuwa wanapeana zilikuwa nzuri na walikuwa na ushirikiano mkubwa kila mmoja alitaka kumpa nafasi mwenzake, walijituma na walijua nini wanafanya, nimefurahi mno,” alisema.

Pluijm alisema, ingawa hawakuweza kuonekana fiti kipindi chote cha dakika 90 lakini hiyo ni hali ya kawaida kwa wachezaji, hata wa Barcelona na timu nyingine za Ulaya kuna wakati wanakuwa sawa na kipindi kingine wanapunguza mashambulizi lakini hawaharibu mchezo.

Alisema wachezaji wake wanazidi kuwa bora kila wakati na kila wanapoingia uwanjani na huo ndio mpango wake aliojiwekea kuhakikisha anaiona Yanga ikifanya vizuri kwa kila mchezo.

“Kila mmoja ameona mchezo waliouonyesha na hivi ndivyo timu inavyotakiwa kuwa, nataka mabadiliko ya kila siku na ushirikiano,” alisema.

Kuhusiana na kukosekana kwa mchezaji wake Haruna Niyonzima ambaye amesimamishwa na uongozi kutokana na kudaiwa kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu alisema kila mchezaji kwake ana uwezo wa kuisaidia timu hivyo hawezi kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja.

Baada ya ushindi huo wa juzi, Yanga imeendelea kuwa kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu huku ikiwa imejikusanyia pointi 30.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles