23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda: Ujenzi wa maabara palepale

PM-PINDANa Mwandishi Wetu, Mwanza
WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda amesema tarehe ya mwisho iliyotolewa na Serikali ya kusimamia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari iko palepale na amewataka watendaji wa halmashauri na mikoa kuhakikisha wanatimiza agizo hilo.

Alitoa agizo hilo Mwanza jana alipozungumza na watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waratibu wa Elimu wa Wilaya na Mikoa waliohudhuria ufunguzi wa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano hayo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, alisema Serikali haijalegeza msimamo wake.

“Juni 20, mwaka huu bado iko palepale, wakuu wa mikoa na wilaya simamieni shughuli za ujenzi zikamilike kwa wakati,” alisema Pinda.

Alisema mbali na maabara, Serikali bado inakabiliwa na changamoto ya kumaliza tatizo la uhaba wa madawati.

Kutokana na hali hiyo, alizitaka halmashauri ziendelee kutenga fedha kila mwaka na kushirikiana na taasisi zinazosaidia jitihada za Serikali kupunguza tatizo hilo kuhakikisha linakwisha nchini.

Pinda alitumia fursa hiyo kuzungumzia tatizo la mipaka ya shule na utunzaji wa mazingira ya shule na kuwataka wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya kusimamia kwa ukamilifu suala hilo.

“Simamieni maeneo yote ya shule yapimwe na yawe na hatimiliki. Lakini wakati wa ujenzi wa shule zetu hakikisheni ramani za shule zinazingatia kuwapo viwanja vya michezo ili wanafunzi waweze kufanya mazoezi na kucheza,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles