24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda: Namaliza utumishi wangu salama

PM-PINDANA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kumaliza salama utumishi wake serikalini.

Akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki wakati wa Ibada ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Anna iliyoko Hananasifu, Kinondoni Dar es Salaam jana, Waziri Mkuu Pinda alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa amelitumikia Taifa kwa miaka 15 akiwa katika nafasi za juu serikalini.

“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kulitumikia Taifa nikiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na miezi tisa na pia katika ngazi ya uwaziri kwa miaka miwili na nusu na miaka mitano nikiwa Naibu Waziri.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumaliza uongozi wangu serikalini. Ninamaliza uongozi wangu kwa amani na furaha. Katika ibada hii ya shukrani, nimemuomba Mungu anisamehe kwa matamshi niliyoyatoa nikiwa kiongozi kwani mengine yanaweza kuwa yaliwaudhi watu bila mimi kujua.

“Uwaziri Mkuu ni kazi ngumu yenye changamoto nyingi, nitakuwa mtu wa ajabu nisipomshukuru Mungu kwa uongozi wake katika kipindi chote hicho tangu nikiwa Naibu Waziri hadi kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu.

“Wito wangu kwa Watanzania wote ni kwamba, msiache kumtaguliza Mungu maishani kwa sababu yeye ndiye mtoaji wa yote, wote tuendelee kumtii Mungu na viongozi wetu wa kiroho kwa sababu wako hapa kumwakilisha yeye.

“Kuna baadhi ya watu wakipata madaraka wanaona kwenda kanisani ni kero au ni kupoteza muda, tatizo lao ni kutojijua, hawatambui kwamba bila Mungu hizo nafasi wasingezipata.

“Ninawaomba tujue kwamba kuna maisha hata nje ya utumishi wa umma na utumishi wa kisiasa,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Alisema katika utumishi wake wa umma, amejifunza mambo mengi lakini kikubwa alichobaini ni kujua jinsi ya kuishi na watu.

Alitumia fursa hiyo kumshukru mke wake, Mama Tunu Pinda kwa kuwa nguzo ya familia na kuwalea watoto wote walionao wakati yeye akihangaika na masuala ya kitaifa.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza la Walei la Parokia hiyo, Arbogasti Warioba, alisema wao wanamshukuru Mungu kwa ulinzi aliompatia Pinda kwa kipindi chake chote cha uwaziri mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles