28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda ajiandikisha kijiji kwake Katavi

prime-ministerNa Mwandishi Wetu, Mpanda
WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda amewataka Watanzania watumie fursa ya uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa kujiandikisha waweze kushiriki uchaguzi mkuu ujao Oktoba 25 mwaka huu.
Hayo aliyasema jana baada ya kujiandikisha kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata katika Kijiji cha Kibaoni wilayani Mpanda, Mkoa wa Katavi.
“Ninawasihi Watanzania wote tusiache kutumia fursa hii… kila mtu ahakikishe anajiandikisha. Ni fursa pekee itakayohakikisha kila mwananchi anashiriki uchaguzi wa kumpata rais, mbunge na diwani,” alisema Pinda.
Waziri Mkuu alisema amefarijika kwa kazi aliyoiona ikifanyika ambako hadi sasa Halmashauri za Nsimbo na Mlele zimeandikisha watu kwa zaidi ya asilimia 100.
Mapema, akiwasilisha taarifa ya uandikishaji katika Halmashauri ya Mlele, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Godwin Benne, alisema walilenga kuandikisha watu 19,482 lakini hadi kufikia jana waliandikisha watu 20,292 ambao ni asilimia 105.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles