27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Pigo kubwa kwa Rais Trump wa Marekani Maseneta wanamtaka abadilishe siasa yake kuelekea Saudi Arabia

OTHMAN MIRAJI, UJERUMANI

RAIS Donald Trump wa Marekani amepata pigo kubwa. Baraza la Senate la Bunge +-(Congress) lenye wawakilishi kutoka mikoa yote ya nchi limepiga kura kwa sautimoja kuunga mkono azimio lenye kumtaja Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia,Mohammed bin Salman, kuwa anabeba dhamana ya kuuliwa Mwandishi wa Habari Jamal Khashoggi. Kwa hakika, kura hiyo ilikuwa alama na ilitoa ishara.

Hatahivyo, kwamba azimio hilo limeungwa mkono kwa mapana na marefu ni pigo kubwa kwa siasa ya kigeni ya Rais Trump. limewapa haki maseneta wa Chama cha Democratic na wale walio marafiki wa rais kutoka Chama  cha Republican ambao wanataka mabadiliko ya kimsingi yafanywe katika siasa yaMarekani kuelekea Saudi Arabia.

Chakushangaza ni kwamba pia maseneta wengi waliliunga mkono azimio lingine lililotaka upunguzwe msaada wa kijeshi kwa Saudi Arabia. Maseneta 57 walitaka usitishwe ushirikiano wa Marekani kwa Saudi Arabia katika Vita vya Yemen: kuacha kuwafunza marubani wa kijeshi wa Saudia, kusita kuipatia nchi hiyo ya Kiarabu habari za siri juu ya vita vya Yemen na kusita kuipatia vifaa vya kijeshi. Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na hali ya sasa ambayo haiendani na malengo ya ushirikiano huo.

Hasa maseneta wamelaumu kukosekana uwazi katika suala la kuuliwa hapo Oktoba 2, mwaka huu Mwandishi wa Habari na mpinzani wa utawala wa Riyadh, Jamal Khashoggi, ndani ya jengo la Ubalozi Mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul,Uturuki. Vidole vimeelekezwa kwa makachero wa Kisaudi kwamba ndio waliofanya mauaji hayo.

Ni Seneta Bob Corker, anayeacha wadhifa wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Kigeni ya Baraza la Senate, aliyewavutia wenzake mbalimbali wamtake Rais Trump abadilishe siasa yake kuelekea Saudi Arabia. Kilichowashangaza wachunguzi wa mambo ni kwamba Corker aliweza kuungwa mkono na kiongozi wa maseneta wa Cham acha Republican, Mitch McConnell.

Kwa muda mrefu kati ya wabishi wa siasa za Trump ni pia Lindsey Graham. Seneta huyo mwenye umri wa miaka 63 na ambaye kwa siku kadhaa  alieleza namna alivyokasirishwa na Mwanamfalme Mohammed bin Salman, alisema: Hatuwezi kuendelea kufanya kama vile hamna kitu kilichotokea. Mwanasiasa huyo aliyekuwa msiri wa Trump kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kwamba huenda akateuliwa kuwa Waziri wa Sheria. Sasa yaonesha anachukua msimamo wa kupambana na Ikulu ya Washington.

Upinzani wa Baraza la Senate dhidi ya Rais sasa umefikia kiwango cha kihistoria. Ni mara ya kwanza kwa Baraza la Bunge (Congress) kutaka wanajeshi wa Kimarekani waondoshwe kutoka medani ya vita kwa kutumia Sheria ya Mamlaka ya Vita (WarPower Act) ambayo kikatiba imeleta mabishano, lakini mwishowe iliruhusu kuendelezwa Vita vya Vietnam.

Licha ya hayo, hisia za maseneta na wananchi wa Marekan ni wazi kabisa, hasa tangu pale Mkurugenzi wa Wakala wa Ujasusi wa nchi hiyo (CIA), Gina Haspel, alipokiarifu kikundi kidogo cha maseneta namna anavyotathmini kisa cha kuuliwa Khashoggi. Maelezo yake yameonesha kwamba madai yanayoelekezwa dhidi ya Riyadh hayawezi kuzuilika na kupuuzwa. Hasa Seneta Corker alisema wazi mbele ya kamera: IKiwa Mrithi wa Mfalme (Mohammed bin Salman) atalazimika kusimamama hakamani, basi baada ya tu dakika 30 atapatikana na hatia na kuhukumiwa.

CIA inachukulia kwamba Mohammed bin Salman yuko nyuma na amehusika na uhalifu uliofanywa. Kama ushahidi kuna mazungumzo kadhaa ya simu. Gazeti la Marekani la Washington Post, ambalo Khashoggi alikuwa analiandikia makala kwa muda, liliripoti kwamba Wakala wa CIA una hakika kwamba haiwezekani kwa makachero wa Kisaudi waendeshe mauaji katika nchi nyingine bila ya Mrithi wa Mfalme kujua.

Haifikiriwi, lakini, kwamba Donald Trump atavutiwa na ataikubali tathmini hiyo ya CIA. Jumanne iliyopita Rais huyo alisisitiza mbele ya waandishi wa habari: Bin Salman ni kiongozi wa Saudi Arabia. Kama mshirika wa karibu wa Marekani, nchi hiyo (Saudi Arabia) ina umuhimu mkubwa wa kimkakati katika eneo hilo (laMashariki ya Kati). Zaidi ya hayo ni kwamba Riyadh ni mteja mwenye fedha nyingi kwa viwanda vya silaha vya Marekani.

Linapokuja suala la hela na haki za binadamu, Donald Trump ameweka wazi upande gani anasimama. Angalau hilo watu wanalijua. Hajatafuna maneno, licha na lolote liwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles