MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
JUMLA ya wafanyabiashara sita akiwemo Balozi wa baa ya Liquid Pub iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam, Piere Gumbo maarufu Liquid Master wamejishindia mamilioni katika droo ya tatu ya promosheni ya ‘Shinda Mtaji’ inayoratibiwa na Kampuni ya Selcom na Mastercard huku lengo kuu likiwa ni kuongezea mitaji na kukuza biashara zao.
Promosheni hiyo iliyozinduliwa rasmi Novemba mwaka jana imelenga wafanyabiashara wote nchini ambao wanaendelea kujiunga na kutumia huduma ya Master pass QR katika kupokea malipo mbalimbali kwenye biashara zao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika makabidhiano ya hundi kwa washindi hao, Meneja Masoko wa Selcom, Juma Mgori amesema promosheni hiyo inawezesha kushinda milioni moja kila wiki kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Novemba hadi Januari 2018.
“Master pass QR ni huduma inayomuwezesha mteja kufanya malipo ya bidhaa na huduma mbalimbali kutoka kwenye akaunti ya simu au akaunti ya benki kwa kuingiza Pay Number ya mfanyabiashara au ku-skani kodi ya QR iliyopo kwenye eneo la mfanyabiashara kwa kutumia simu ya Smartphone,” ameeleza.
“Kupitia huduma ya Masterpass QR, mteja ataweza kufanya malipo kupitia mitandao ya simu kutoka Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, Halopesa, Ezypesa na Selcom Card. Pia kwa upande wa huduma ya mobile banking ataweza kufanya malipo kutoka Access Bank, I&M Bank, NBC Bank, Akiba Commercial Bank, Amana Bank, BancABC, Canara Bank, Exim Bank, TPB Bank, NMB Bank, FINCA Microfinance Bank na Standard Chartered Bank” alisema.
Mmoja wa washindi hao Gerald Moshi anayewakilishi kampuni ya Moshi Shop iliyopo Arusha, alitoa wito kwa wafanyabiashara kuchangamkia huduma ya Masterpass QR kwa kuwa inalenga kuwaondolea watanzania adha ya kubeba fedha taslimu au kuwa na kadi ya benki muda wowote wanapohitaji kufanya malipo.
Wafanyabiashara wengine waliojishindia milioni moja kila mmoja ni Faraji Hardware, kampuni ya Irene Designing