24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watetezi haki za binadamu waanzisha operesheni ‘Tetea Haki za Mtuhumiwa’

Asha Bani, Dar es Salaam

Watetezi wa Haki za Binadamu nchini wameungana na kuzindua operesheni maalumu ya ‘Tetea Haki za Mtuhumiwa’ nchi nzima wakianza na Mkoa wa Arusha wilayani Ngorongoro.

Watetezi hao ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), ambao wamesema lengo lao ni kupambania  waathirika wa matukio ya watu kukamatwa na kukaa mahabusu bila hatia.

Pia  wameitaka Serikali na uongozi wa juu wa Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali za kisheria askari Polisi waliohusika na ukatili mbalimbali kwa baadhi ya watuhumiwa hasa waliokamatwa hivi karibu huko Loliondo ambao baadaye waliachiwa mwishoni mwa wiki.

Wamewataja wananchi hao waliowekwa mahabusu kwa wiki nzima kuwa ni pamoja na Peter Orkery, Musa Yahya, Kayanda Kisoki, Zakaria na Francis Arusha ambao walikamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani Ngorongoro tangu Desemba 21, mwaka jana hadi Januari 4, mwaka huu.

Akitoa tamko lao leo Jumanne Januari 22, jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari,  Mratibu wa Kitaifa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema licha ya kukaa wiki nzima lakini pia walifanyiwa vitendo vya kikatili jambo ambalo halifai katika taifa.     

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles