25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Basata yawafungulia Diamond, Rayvanny na Wasafi Festival

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewafungulia wasanii kutoka kundi la Wasafi Nasib Abdul (Diamond Platnumz) na Raymond Mwakyusa baada ya kufungiwa kutokujihusisha na shughuli zozote za sanaa kwa kipindi kisichojulikana kutokana na sababu za kimaadili.

Pamoja na kuwafungulia wasanii hao baraza hilo pia limeruhusu kufanyika kwa tamasha la Wasafi ambalo nalo lilifungiwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza Jumatatu Januari 22, imesema baraza limefikia uamuzi huo baada ya kupokea maombi kadhaa kutoka kwa wasanii hao na Kampuni ya Wasafi (WCB).

Taarifa hiyo imesema baada ya kupokea maombi yaliwasilishwa kwa Mwenyekiti wa Bodi ya baraza hilo na kwa kuzingatia jukumu la Basata la kusimamia, kuendeleza na kukuza wasanii na sekta ya Sanaa nchini, Baraza limeamua kuwaruhusu wasanii hao waendelee na shughuli zao.

“Tutaendelea kufuatilia kwa karibu kazi za wasanii hawa na WCB kiujumla ili kuhakikisha wanazingatia maadili,” imesema taarifa hiyo.

Ikumbukwe kuwa Desemba 18 mwaka 2018, Basata iliwafungia wasanii hao kufanya onyesho lolote ndani na nje ya nchi baada ya wawili hao kuonesha utovu wa nidhamu kwa kutumbuiza wimbo wao wa kushirikiana unaojulikana kwa jina la Mwanza katika tamasha la Wasafi bila kujali kama wimbo huo ulifungiwa na Baraza hilo kwa kukosa maadili, huku wakiagiza tamasha hilo pia kutofanyika nchini.

Aidha baada ya Basata kuwafungulia Diamond Platnumz alituma ujumbe wa kuishukuru Wizara ya Sanaa, Habari, Utamaduni na Michezo na Basata kwa kuwaruhusu kufanya kazi zao tena huku akisema ni muda muafaka wa wao kuachia wimbo mpya kwa mwaka huu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles