26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Picha za faragha zamponza Wema Sepetu, serikali yamfungia kwa muda usiojulikana

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Bodi ya Filamu nchini imemfungia msanii wa filamu ‘Bongo Movie’ Wema Sepetu, kutojishughulisha na masuala ya filamu kwa muda usiojulikana kutokana na picha zake za faragha kusambaa katika mitandao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na bodi hiyo, hatua hiyo inatokana na ukiukwaji wa sheria ya filamu na michezo  ya kuigiza Namba 4, ya mwaka 1976 na kanuni zake Na. 156 za mwaka 2011.

“Kifungu cha 27 cha kanuni hiyo kinalekeza mtu yeyote atashiriki kwa namna yoyote au kuonesha au kusababisha mtu yeyote kuangalia picha jongefu inayokinzana na masharti ya kanuni za sheria ya filamu atakuwa amekiuka sheria hizo.

“Aidha kanuni ya 24, kifungu cha 1, vifungu vidogo vya (c), (d), (j), (k), na (u), ambavyo vinaeleza kuhusu suala la kudhalilisha heshima na utu  kuvunja ushirikiano wa kimataifa huwafanya watazamaji waige tabia mwenendo, desturi na maadili yasiyofaa na wakiuke maadili yaliyo katika utamaduni wa Tanzania na ludhalilish ataifa kwa ujumla,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, bodi hiyo imetoa onyo  kwa wanatasnia wote  wa filamu na michezo ya kuigiza wenye tabia kama hizo kuacha mara moja na endapo watauka hawatasita kuchukua stahiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles