24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Mama Samia awataka wakazi Kisarawe kulinda miundombinu ya maji

Na TUNU NASSOR – DAR ES SALAAM


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wakazi wa wilaya ya Kisarawe kuhakikisha wanalinda miundombinu ya mradi wa maji ili udumu.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea mradi wa maji wa Kisarawe, Samia alisema wakiulinda mradi huo utaweza kuondoa kabisa shida ya maji katika mji huo.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kutaweza kuimarisha ustawi wa viwanda katika wilaya hiyo.
“Matunzo na ulinzi wa mradi huu ni juu yenu, mkiutunza hakutakuwa na shida ya maji na kuimarisha ustawi wa viwanda na kuongeza ajira,” alisema Samia.

Alisema anaipongeza wizara ya maji na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), kwa jitihada za kuongeza upatikanaji maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

“Nimekuwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa (mhandisi Cyprian Luhemeja) ambaye amenieleza jitihada za kuleta maji Pwani na Dar es Salaam,” alisema Samia.

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia wilaya ya Kisarawe kupata maji kwa asilimia 100.

“Mradi huu utagharimu Sh Bilioni 10.864 ambapo Dawasa itagharamia mradi huu kwa asilimia 100,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema kwa sasa Dawasa imeanzisha akaunti maalumu yavuwekezaji ambapo mpaka sasa ina Sh Bilioni 4.5.

“Tumejiwekea Utaratibu wa kuweka asilimia 35 ya Mapato ya Dawasa kupelekwa katika uwekezaji ili kuziwezesha mamlaka za maji hasa grade A kujitegemea,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema mkandarasi anayetekeleza mradi huo alitakiwa kutumia miezi 15 kumaliza mradi lakini yeye amekubaliana naye atumie miezi nane tu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,207FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles