24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Pep Guardiola alia na VAR

MANCHESTER, ENGLAND

BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City kulazimishwa sare ya mabao 2-2 kwenye uwanja wa nyumbani Etihad, kocha wa timu hiyo Pep Guardiola ameutupia lawama mfumo wa VAR.

Kocha huyo amedai mfumo huo una faida kubwa lakini waamuzi wamekosa umakini hasa baada ya timu yake kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji wake Gabriel Jesus na kisha kukataliwa na kuufanya mchezo huo umalizike kwa sare.

Hii sio mara ya kwanza kwa kocha huyo kuutupia lawama mfumo huo, msimu uliopita kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wapinzani hao aliulalamikia mfumo huo baada ya mchezaji wa Tottenham kufunga bao ambalo mkono wake uligusa mpira kabla ya kufunga, lakini mwamuzi aliita kati japokuwa aliangalia kwenye VAR.

Baada ya tukio hilo la juzi, kocha huyo aliongea kwa utani huku akisema, wakati tukio hilo linatokea VAR ilikuwa ipo mapumzikoni.

“Hatukustahili kupata penalti katika dakika 45 za kipindi cha kwanza? Ninaamini tulikuwa na nafasi hiyo, lakini siwezi kuliongelea hilo labda akaulizwe bosi wao wa mfumo huo jijini London.

“Lilikuwa tuta la wazi kwa kitendo kilichofanywa na Erik Lamela wakati anapambana na Rodri, labda wakati tukio hilo linatokea VAR ilikuwa mapumzikoni ikipata kahawa.

“Kwa nini haikuwa mpira uliufuata mkono kwa Fernando Llorente kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katika hatua ya robo fainali msimu uliopita, lakini katika mchezo huu wa leo imepitishwa kwa nini?

“Inaumiza sana kwa kuwa lilikuwa bao letu katika dakika za mwisho za mchezo na tulitakiwa kuongeza mchezo huo, tulionewa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na leo tunaonewa tena? Ni jambo la kuwaachia watu wenyewe wa VAR,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles