27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Gareth Bale ahakikishiwa kubaki Madrid

MADRID, HISPANIA

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amethibitisha kuwa, mshambuliaji wake Gareth Bale ataendelea kuwa ndani ya kikosi hicho katika kipindi hiki cha msimu mpya wa Ligi.

Kauli hiyo iliitoa mwishoni mwa wiki baada ya mchezaji huyo kuwa kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo wao wa ufunguzi michuano ya Ligi Kuu Hispania dhidi ya Celta Vigo ambapo Madrid walishinda mabao 3-1.

Bale alikuwa kwenye kikosi hicho baada ya mshambuliaji wao mpya Eden Hazard kuwa nje ya kikosi baada ya kuumia, lakini Bale alikuwa kwenye mchango wa bao lililofungwa na mshambuliaji wao Karim Benzema.

Hata hivyo Bale alionekana kuhusika kwenye mabao mengine ya mchezo huo yaliyofungwa na Toni Kroos na Lucas Vazquez.

Wakati huu wa uhamisho wa wachezaji Bale alitajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji ambao wanatakiwa kuondoka kutokana kutokuwepo kwenye mipango ya mwalimu huyo na alikuwa anahusishwa kutaka kutimkia katika Ligi ya nchini China.

Hata hivyo, Zidane alithibitisha kuwa, Bale lazima aondoka wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi baada ya mchezaji huyo kuachwa nje ya kikosi katika michezo mbalimbali ya kirafiki.

Lakini baada ya mchezo huo wa juzi, Zidane amedai mchezaji huyo ataendelea kuwepo kikosini katika msimu huu mpya.

“Ataendelea kuwa kikosini, kwa sasa kitu kikubwa cha kukiangalia ni maendeleo ya msimu huu na sio vinginevyo.

“Kuumia kwa Hazard ni bahati mbaya kwetu, lakini haiwezi kubadilisha malengo tunayo Bale kwenye kikosi ambaye anaweza kuziba nafasi hiyo, ninaamini Bale, James Rodriguez na wengine wataipigania timu hii,” alisema kocha huyo.

Baada ya ufunguzi wa Ligi hiyo, Madrid wapo kileleni huku wakiwa na pointi tatu, wakati huo mabingwa watetezi Barcelona wakiwa hawana pointi baada ya kupoteza mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Athletico Bilbao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles