27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Pedro: Nataka kurudi Barcelona

 Pedro Rodriguez
Pedro Rodriguez

LONDON, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa pembeni wa klabu ya Chelsea na timu ya Taifa ya Hispania, Pedro Rodriguez, amesema yupo tayari kurudi katika timu yake ya zamani, Barcelona.

Mchezaji huyo alisajiliwa na Chelsea akitokea Barcelona Agosti 2015, lakini amedai kwamba tayari ameanza kufanya mazungumzo na rais wa Barcelona, Josep Bartomeu, kwa ajili ya kutaka kurudi kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Pedro amedai hajutii kujiunga na klabu ya Chelsea, lakini anaamua kutaka kurudi Barcelona kwa kuwa amewakumbuka wachezaji wenzake na anataka kumaliza soka lake katika klabu hiyo.

“Ninaamini nitarudi Barcelona, najua ni ngumu lakini itawezekana kwa kuwa tayari nimefanya mazungumzo na rais wa klabu hiyo pamoja na watu wengine ambao wanapenda kuniona nikiwa katika klabu hiyo.

“Si jambo rahisi lakini nakumbuka niliwahi kusema kwamba nataka kumaliza soka langu katika klabu hiyo. Kila siku timu hiyo inakuwa na wacheza wenye uwezo wa hali ya juu hivyo inakuwa ngumu kupata nafasi, lakini ninaamini bado nafasi yangu ipo na nitamalizia soka langu hapo.

“Nimetumia miaka 11 au 12 nikiwa Barcelona, familia yangu ipo pale, rafiki zangu wapo wengi, mashabiki ambao wananikubali, hivyo ni ngumu kuachana na klabu ya ndoto yako,” alisema Pedro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles