25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Peaktime Media yaahidi burudani kabambe ya masumbwi

NA WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

UONGOZI wa kampuni ya Peaktime Media ambao ni waandaaji wa mapambano ya ngumi nchini, umehidi kutoa burudani kabambe kwa mashabiki wa masumbwi mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Meja Seleman Semunyu jana baada ya kufuturisha mabondia na wadau wa ngumi kwenye Ukumbi wa JWTZ (Club 361) uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

Meja Semunyu amesema katika kuhakikisha burudani hiyo inawafikia Watanzania wengi, kwa mara ya kwanza historia itaandikwa Songea, mkoani Ruvuma ambapo pambano la kisasi ya marudiano litapigwa kati ya Selemani Kidunda na Erick Katompa Julai 30,2022.

Baadhi ya wadau waliojitokeza katika futari iliyoandaliwa na Peaktime Media jana

“Tulianza na Mfalme kwenye Ufalme wake(Twaha Kiduku Vs Alex Kabangu) Morogoro, sasa tutakwenda Songea kwenye Usiku wa Kisasi 2022 kati ya Kidunda na Katompa, pambano hili tayari Mkuu wa Majeshi ameshatoa kibali, naamini mtaendelea kuniunga mkono,” amesema.

Selemani Kidunda(kulia) na Erick Katompa(kushoto),waliopo vifua wazi walipokutana mwaka jana.

Meja Semunyu amefafanua kuwa tangu mwaka jana hadi sasa, wamefanikiwa kuandaa mapambano 10, hivyo anaamini wadau wa ngumi watazidi kumpa sapoti ili kufanikisha malengo waliyojiwekea katika kuendeleza mchezo wa masubwi.

Kwa upande wake, Kidunda amesema yeye yupo vizuri na anaendelea na mazoezi, huku makocha wake wakiendelea kumnoa na kurekebisha pale walipokosea, hivyo atahakikisha ubingwa unabaki nyumbani.

Baadhi ya wadau waliojitokeza katika futari iliyoandaliwa na Peaktime Media jana

“Tulilotaka liwe limekuwa, ndio kama hivi mnaona Mcongo anarudi tena, kama vile usemi wangu kuwa ‘Ajavyo ndivyo Tumpokeavyo’, naomba tushirikiane katika hii game tuwe pamoja kule Songea,” amesema

Kidunda na Katompa wanarudiana baada mwaka jana kushindwa kupatikana mshindi kutokana na pambano kusitishwa utokana na Kidunda kuumizwa kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles