25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Pacquiao atawaachia Wafilipino zawadi ya ushindi leo?

PacquiaoLAS VEGAS, Marekani

MKALI wa ngumi nchini Ufilipino, Manny Pacquiao, leo anatarajia kushuka ulingoni kwa ajili ya pambano lake la mwisho dhidi ya mpinzani wake, Timothy Bradley, raia wa nchini Marekani.

Hili litakuwa pambano lake la kwanza tangu Pacquiao apokee kichapo kutoka kwa bingwa wa mchezo huo, Floyd Mayweather, Mei mwaka jana kwenye ukumbi wa MGM Grand Arena.

Pambano la leo ni kugombania ubingwa wa Welterweight, ambapo kutakuwa na raundi 12. Pacquiao aliweka wazi mapema baada ya kupigwa na Mayweather ambapo alidai kwamba anahitaji pambana la mwisho ili aweze kuachana na mchezo huo.

Litakuwa ni jambo la aibu kwa bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 akatangaza kustaafu huku akiwa amepokea kichapo cha pili mfululizo, ila ni vizuri kama ataweza kushinda pambano la leo kwa ajili ya kujiwekea heshima nchini Ufilipino pamoja na duniani kote.

Nchi ya Ufilipino leo hii inaungana pamoja kwa ajili ya kumpa sapoti shujaa wao katika pambano la leo ili aweze kumaliza salama na kwa ushindi kama alivyopewa sapoti katika pambano lake dhidi ya Mayweather japokuwa alishindwa.

Katika pambano la leo bondia huyo amedai kwamba ushindi kwake utakuwa ni zawadi tosha kwa wananchi wa nchini Ufilipino kutokana na mchango wao mkubwa ambao waliuonesha katika maisha yake ya ngumi.

“Kama nitafanikiwa kushinda katika pambano hilo basi litakuwa jambo muhimu katika maisha yangu na zawadi kubwa kwa wananchi wa nchini Ufilipino.

“Ninaamini nina nafasi ya kushinda kutokana na maandalizi ambayo nimeyafanya kwa kipindi chote, hivyo nahitaji sapoti ya wananchi wangu na mashabiki wangu wote duniani,” alisema Pacquiao.

Bondia huyo alidai kwamba akimaliza pambano hilo atawaaga mashabiki wake wa ngumi na kurudi nchini Ufilipino kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wake katika masuala ya siasa.

Ndoto zake

Bondia huyo alikuwa na ndoto za kuwasaidia wananchi wa Ufilipino katika kutetea haki zao, alidai kwamba watu wa nchi hiyo wamekuwa wakionewa sana na mataifa mbalimbali.

Kutokana na hali hiyo huku akiwa na umri wa miaka 15, aliamua kujifunza ngumi kwa ajili ya kupigania haki za watu wa Ufilipino.

Amewafanyia nini

Tayari amekuwa balozi mzuri wa ngumi duniani kutokana na kila ambacho amekifanya katika mchezo huo kwa kutwaa ubingwa wa aina mbalimbali na kuitangaza nchi hiyo.

Hata hivyo, amekuwa akitetea haki za wananchi wa Ufilipino kutokana na uwakilishi wake katika masuala ya kisiasa na ndio maana wanamuunga mkono na wananchi wote.

Anatarajia kuwafanyia nini

Bondia huyo amedai kwamba anataka kuwapa ushindi wa pambano la leo dhidi ya Bradley ambapo tayari wananchi wanausubiria kwa hamu huku wengine wakiwa tayari wamefika nchini Marekani kwa ajili ya kushuhudia ubingwa huo unavyochukuliwa.

Je, ataweza kutwaa ubingwa huo leo au itakuwa kama Mei mwaka jana kwa kuweka kisingizio kwamba alipatwa na maumivu ya bega wiki mbili kabla ya pambano? Ngoja tuone.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles