27.8 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Pacquiao ajiandaa na pambano lake

pacq_3115733bLOS ANGELES, MAREKANI

BONDIA Manny Pacquiao, juzi aliwasili jijini Los Angeles nchini Marekani kwa ajili ya kujiandaa na pambano lake dhidi ya Timothy Bradley Jr.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 37, anatarajia kufanya mazoezi ya nguvu kwa wiki tatu kwa ajili ya pambano hilo ambalo litakuwa la mwisho kabla ya kustaafu.

Pambano hilo linatarajia kufanyika Aprili 9 mwaka huu, huku likiwa ni pambano lake la kwanza tangu apigwe na bingwa wa mchezo huo, Floyd Mayweather, Mei mwaka huu kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden, uliopo Las Vegas.

“Mazoezi yangu wakati nipo nchini Ufilipino yalikuwa mazuri sana, lakini kwa sasa nimeamua kuja kumalizia huku Hollywood kabla ya pambano hilo.

“Najua mashabiki wana maswali mengi sana ila majibu yao yatajibiwa baada ya kumalizika kwa pambano hilo,” alisema Pacquiao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,383FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles