28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

P. Diddy amuomba msamaha kocha wa mtoto wake

Rapper Sean "Puffy" CombsLOS ANGELES, Marekani

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Sean Combs ‘Puff Daddy’, amemuomba msamaha kocha wa mtoto wake baada ya kugombana naye miezi miwili iliyopita.

Diddy aligombana na Sal Alosi baada ya kocha huyo kupishana maneno na mtoto wake wakiwa mazoezini, ambapo Diddy alichukua uamuzi wa kumpiga na kifaa kizito kocha huyo lakini baada ya kuomba radhi akaapa kutokwenda tena mazoezini kumwangalia mwanawe.

“Nilipishana maneno na kocha wa mwanangu, lakini kila kitu kipo sawa kwa sasa na nimemwambia kuwa siwezi kwenda tena kuangalia mazoezi yao.

“Nilimuona kocha huyo wakipishana maneno na mtoto wangu na mimi sikuuliza nikafanya nilichofanya na ninaamini sikuwa sahihi,” alisema Diddy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles