PARIS, Ufaransa
STRAIKA wa Lille, Victor Osimhen, anatamani kusakata kabumbu huku akisisitiza yupo tayari kurejea dimbani.
“Natamani kuingia dimbani tena, nimewakumbuka mashabiki, napenda wanapiga kelele na kuimba nyimbo, nina imani tutarejea hivi karibu,”alisema Osimhen.
Osimhen amefunga mabao 18 katika mashindano yote msiumu huu.
Staa huyo anakipiga katika timu ya taifa ya Nigeria almaarufu Super Eagels.