24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

ORXY Gesi yatekeleza ombi la Dk. Mwinyi kwa kukabidhi mitungi 2,000

Mwandishi Wetu, Zanzibar

KAMPUNI ya gesi ya Orxy imetekeleza maombi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kupeleka mitungi 2,000 ya gesi ambayo itagawiwa kwa wananchi wajasiriamali wanawake kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi sambamba na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia nishati safi ya kupikia.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mudrik Ramdhan Soraga (katikati) akiwa pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Zanzibar, Riziki Pembe Juma (wa pili kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Benoite Araman (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Idara ya Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Shabani Fundi (wa kwanza kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya oryx mmoja wa wajasiriamali waliokabidhiwa mitungi 1,000 katika hafla iliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara, Zanzibar.

Akizungumza wakati wa Oryx ikikabidhi mitungi 1,000 kwa ajili ya wajasiriamali wa visiwani Unguja, Zanzibar Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mudrik Ramadhan Soraga amesema anamshukuru na kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kutoa mapendekezo mahususi kwa kampuni ya Oryx gas kuhusu suala la kuwapa nyezo safi na salama wajasriamali wanaofanya shughuli za mama upishi.

“Naomba mfahamu Rais alielekeza hili jambo katika dhana nzima ya kuweka urahisi kwa mjasiriamali mwanamke anapofanya shughuli zake katika jiko basi oryx gasi wasaidie katika kutoa nishati safi.

“Kwa hiyo tumpongeze Rais Dk. Mwinyi kwanza kwa kuja na mawazo hayo lakini kuthubutu kutoa maelekezo kwa Oryx na leo hii tunakutana hapa kutoa mitungi ya gesi ambapo leo tunakabidhi mitungi 1,000 kwa wajasiriamali wa Unguja na wiki chache zijazo itakabidhi mitungi mingine 1,000 kwa wajasiriamali wa wa Pemba,” amesema.

Akieleza zaidi amesema wanawashukuru Oryx wamekuwa wadau muhimu katika sekta ya nishati ndani ya visiwa vya Zanzibar hususan katika kufanikisha ajenda ya kutumia nishati mbadala katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku katika majumba yao.

Ameongeza kuwa Oryx kwa kipindi cha muda mfupi wamekuwa na kampeni endelevu ya kuhakikisha matumizi ya gesi safi na salama yanapewa kipaumbele sambamba na kumuunga mkono Rais Dk. Mwinyi katika malengo yake ambayo amekusudia ya kuifanya Zanzibar kuwa ni sehemu inayotumia gesi katika shughuli zake zote za kiuchumi.

Amesema Serikali ya Awamu ya Nane imekuwa na lengo la kuhakikisha inatoa fursa mbalimbali kwa wananchi wao kuweza kumudu maisha yao kupitia uwezeshaji au kutengeneza mazingira ambayo wenyewe wanaweza kujiajiri.

Amefafanua kuwa kupitia mpango wa uwezeshaji wanancho kiuchumi katika kipindi cha miaka mitatu kumekuwa na mafanikio makubwa na kiasi cha Sh bilioni 27 kimetolewa na Serikali kukopesha wananchi ambapo wajasiriamali wasiopungua 26,000 wamepata mkopo.

“Kwa hiyo tunafarijika tunapoona wadau kama Orxy mnapojumuika kuunga mkono juhudi za Serikali kwani bila ya mashirikiano hayo, kujitoa na kuthamini mchango wa serikali katika jambo hili hatuwezi tupambana na ukosefu wa ajira ambalo ndio adui mkubwa,” amesema.

Ameongeza ni vema juhudi hizo ambazo wanashirikiana na wadau wakiwemo Orxy lazima ziende na kubadilisha mtazamo wa namna tunavyofanya shughuli zao huku akisisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia inakwenda kumpunguzia changamoto mtoto wa kike ambaye amekuwa akitumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa.

“Tumeamuangalia mtoto wa kike na kuona tunamwekea mazingira mazuri ili asilazimike kwenda mbali kutafuta kuni na mkaa, akina baba tuondokane na ile dhana kwamba mtoto wa kike ndio analazimika na kutafuta kuni. Ni lazima tuhakikishe tunawalinda watoto wetu wa kike,” amesema.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania LTD, Benoit Araman amemshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa kuwaalika Zanzibar ili kufikisha nishati safi ya kupikia huku akimpongeza kwa juhudi na kazi kubwa aliyoifanya kuhakikisha Zanzibar inakuwa sehemu kivutio kwa wawekezaji.

“Oryx ilianza kufanya biashara ya kupikia Zanzibar na Pemba mwaka 2016. Oryx Gas Zanzibar ilizinduliwa rasmi Desemba 2021. Hii ni ishara kwanza ya imani katika utawala wake. Tangu kipindinhicho, Rais Mwiny ametupa msukumo mkubwa Oryx Gas kuendelea kuwekeza zaidi visiwani.

“Tumefanikiwa kuwa na mkataba wa ushirikiano kati ya Oryx Gas Zanzibar na Zanzibar Group TP ambao sasa hivi wamekua mdau wetu mwenye asilimia 30. Ushirikiano huu umefanikisha ujenzi wa kituo cha LPG ambacho kita kitakuwa kimekamilika kabla ya robo ya kwanza ya mwaka huu 2024.

“Hili ni jukumu kuu ya Oryx Gas Zanzibar na TP kwa wananchi wa visiwa. Maono ya Rais Dk. Mwinyi pamoja na ujasiri wa Oryx Energies na mshirika wetu TP itaruhusu kufanya usambazaji wa LPG kuwa endelevu na nafuu zaidi kwa wakazi wa Zanzibar na Pemba hatua hii itasaidia kuleta maendeleo bora sekta ya utalii,” amesema Araman.

Ameongeza kuwa Oryx inajivunia kuchangia katika maendeleo ya muda mrefu visiwani Zanzibar huku akitumia nafasi hiyo kueleza kupika kwa gesi kunavyiosaidia kulinda mazingira na kutokomeza ukataji wa miti ili kutengeneza mkaa na kuni.

“Pia ina saidia kulinda afya ya wanawake ambao wanaathirika kwa moshi inayotokana na mkaa na kuni, wanawake wataweza kufanya shughuli nyingine nyingi wakipika kwa kutumia LPG maana watapika kwa haraka bila kuharibu ubora na ladha ya chakula.

“Tokea mwaka 2021, Oryx Gas imekua kampuni kinara na kiongozi katika kuimiza watu kupikia kwa nishati safi ya LPG. Tunajivunia kuwa wa kwanza kuleta nishati hii safi kwa wananchi wa Zanzibar na baada ya wiki kadha tunaeneza na Pemba pia,” amesema Araman.

Hivyo, amesisitiza wamekabidhi mitungi ya gesi 1,000 kwa manufaa ya wananchi wa Unguja na hivi karibuni watakabidhi Pemba mtungi 1,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles