28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Operesheni wauza ‘unga’ yanasa mmoja

sirroNA ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni linamshikilia kijana ambaye hakufahamika jina lake, ambaye ni maarufu kwa kuuza madawa ya kulevya.

Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa kijana huyo alikamatwa katika oparesheni maalumu inayoendelea   Dar es Salaam, ya kuwasaka watu wanaojishughulisha na uuzaji na utumiaji wa mdawa ya kulevya.

Picha za kijana huyo pamoja na mali zake zilisambazwa katika mitandao mbalimbali ya  jamii jana zikionyesha mali zake.

MTANZANIA lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,   Simon Sirro  ambaye alisema   taarifa hizo   hajazipata hivyo alimtaka mwandishi afuatilie kwa Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni.

“Taarifa za tukio hilo bado sijazipata naomba umtafute kamanda wa eneo husika anaweza kukupa ufafanuzi au taarifa za tukio hilo,”alisema   Sirro.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alimtaka mwandishi wa habari hizi kufanya utafiti wa jina la mtuhumiwa  aweze kulifuatilia suala hilo.

“Ndugu mwandishi unanipa taarifa ambazo hata huna taarifa kamili hivyo mimi nashindwa kufuatilia  tukio hilo, naomba ufanye utafiti wa jina la huyo mtuhumiwa unipatie  niweze kujua ukweli wa jambo hilo,”alisema Kamanda Fuime.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles