26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Onyesho la SITE kufanyika Oktoba Dar es salaam

Asha Bani-Dar es Salaam

Bodi ya Utalii nchini (TTB), imetangaza kufanya onyesho la Swahili International Tourism (SITE) litakalofanyika Oktoba 18 mpaka 20 mwaka huu.

Onyesho hilo linalitarajiwa kuhudhuriwa na makampuni mbalimbali ya kitaifa na kimataifa litakalofanyika Mlimani City.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa TTB Devota Mdachi amesema onyesho hilo litahusisha mawakala wa utalii, mawakala wa kupandisha watalii mlimani, biashara za hoteli, kambi za watalii, waendesha utalii wa kitamaduni na biashara zinazohusiana na utalii.

“Waalikwa katika onyesho hilo ni pamoja  na mawakala wa utalii wa kimataifa ,waandishi wa habari za mitandaoni za kutangaza utalii  na msanii Peter Msechu akiwa na bendi yake atashiriki katika kuhamasisha maonesho hayo ikiwa ni pamoja na kuutangaza utalii ndani na nje ya nchi,” amesema.

Mratibu wa onyesho hilo Joseph Sendwa ameyataka makampuni mbalimbali kudhamini maonesho hayo pamoja na kushiriki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles