27.4 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Miaka mitano ya M-Pawa kunufaisha zaidi ya washindi 2000

Mwandishi wetu- Dar es salaam

Benki ya CBA na Vodacom leo Juni 13, wamefanya droo ya kwanza kwa ajili ya promosheni ya kutunza na kulipa madeni wakisherehekea miaka 5 ya huduma ya M-Pawa yenye lengo la kuongeza uhusisho wa watu kwenye huduma za kifedha.

Promosheni hiyo inayokusudiwa kufanyika kwa muda wa wiki 6 imeanza na droo ya kwanza ambayo itatoa jumla ya washindi 340 ambao 40 kati yao wataondoka na mara mbili ya fedha waliyohifadhi kwenye akaunti zao kuanzia Shilingi 1000 – 200,000 na wengine 300 kushinda vocha ya shilingi 5000 kila mmoja.

Akiongea kwenye droo ya kwanza Mkrugenzi Mkuu wa CBA Gift Shoko, amesema M-Pawa ni huduma ambayo inaendelea kuwawezesha watanzania wengi hususani wafanyabiashara wadogo na wanaadhimisha miaka 5 kwaajili ya kuwashukuru wateja wao kwa kuendelea kutumia huduma hiyo.

“Tunaendelea kuhimiza kutunza na kulipa madeni mapema na kuhamasisha watu wasiotumia M-Pawa kuanza kuitumia huduma hii,” amesema.

Promoshenni hiyo itaendelea kila wiki huku kukiwa na washindi wengine 50 wa kila baada ya wiki 2 ambao watashinda zawadi ya simu na mshindi mkubwa ambaye atatangazwa kwenye droo ya mwisho atazawadiwa shilingi milioni 15. 

Droo ya kwanza ilifanyika makao makuu ya CBA, Dar es Salaam na ilisimamiwa na wawakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Humudi Abdul Hussein ambaye ni Afisa Mwandamizi na wawakilishi kutoka CBA Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles