28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Ongezeko la Hitaji la Kitaaluma kwa Vijana katika Kutimiza Njozi Zao

Hebu tafakari kuhusu mambo yafuatayo:

  • Fikiria kijana wako hajafuzu elimu ya shule ya msingi, sekondari au chuo, lakini anahitaji kujiendeleza.
  • Wewe ulimaliza elimu yako ya sekondari, lakini  haukuchaguliwa kwa ajili ya elimu ya juu, na unawaza cha kufanya.
  • Wewe ulianzisha biashara, lakini haikidhi mahitaji yako ya maisha. Unahitaji kuendesha biashara yenye fanaka na yenye kutimiza njozi na malengo yako.
  • Wewe haukupata nafasi ya kutimiza elimu yako ya shule na hukuweza kupata taaluma au stadi za hali ya juu ili kutimiza malengo yako. Sasa umri wa wa shule umepita na huna pesa kwa ajili ya kujilipia masomo. Unawaza cha kufanya.

Haya ni baadhi tu ya maswali walionayo vijana  wakiwa wanajaribu kutatua changamoto zao za maisha. Kutoajiriwa au kuwa na kazi isiyokidhi mahitaji ya kila siku, ni swala lialohitaji kutazamwa kwa umakini. Vijana (kati ya miaka 15 na 35) hujumuisha asilimia 34.7 ya watanzania na hivyo ni kundi kubwa zaidi lenye nguvu kazi katika uchumi wetu inchini kwetu. Kundi hili ndilo lililoathiriwa zaidi na kutokuwa na kazi au kazi zisizokidhi mahitaji yao ya maisha na majukumu katika familia zao.

Kwa vile vijana huchukua muda mwingi katika elimu nadharia, jambo huwa pia sababu mojawapo ya vijana kutokuwa na kazi, kuna vijana wengi wanaotoka nje ya mfumo wa elimu, wakihangaika mtaani na shughuli zisizokidhi mahitaji yao. Hivyo hata kama umri wa vijana huhusianishwa sana na muda mrefu katika taasisi za elimu, idadi ya vijana wanaoshindwa kuendelea na elimu ya juu (kwa sababu iwayo yote) huongezeka kwa kadiri ngazi ya elimu inavyoongezeka. Hata hivyo waandishi wengi huripoti idadi kubwa ya vijana katika hali ya ukosefu ajira, na ajira zisizokidhi mahitaji yao kutokana na elimu au ustadi mdogo – hasa kutokakana na zoefu haba wa kazi – walionao. Hili pia huwazuia kuanzisha biashara yenye mafanikio au kupata kazi inayokidhi mahitaji yao ya kiuchumi.

Kituo chetu cha ushauri chenye jina „Consultation Centre for Societal Nurturing“ [yaani: kituo cha ushauri kwa ajili ya ustawi wa jamii] kimejikita katika kushughulika na (hitaji) pengo hili na kutoa msaada kwa vijana wanaohitaji „kujikomboa“ na umasikini na kutimiza ndoto zao za maisha. Huduma hii huhusisha upana unaohitajika kwa kutoa ushauri, kutoa mwongozo, na kushirikiana na wataalamu na taasisi zingine ili kuwaandaa vijana katika kutimiza malengo yao. Tunawaalika kuwasiliana nasi kupitia barua namba ya simu 0784 462140  au barua pepe hii: [email protected]

Karibuni!
Peter Bulengela (Mkurugenzi)

www.societalnurturing.com

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles