25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Omog atangaza ubingwa Msimbazi

 Joseph Omog
Joseph Omog

ADAM MKWEPU, DAR Na EVANCE KIGANJA-(TUDARCO)

KOCHA Mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Omog, amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa kikosi hicho kitanyakua ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Omog alitoa kauli hiyo kutokana na timu hiyo kuanza vyema Ligi Kuu kwa kushinda mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Omog alisema mikakati yao katika kufanikisha lengo la kutwaa ubingwa  ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo watakaocheza kwenye ligi hiyo.

Alisema Simba imesajili wachezaji wengi wenye uwezo hivyo atawapa mbinu za kupambana uwanjani na kuwajengea morali wakati wa mazoezi na mechi zinazowakabili.

“Tunaendelea kuboresha safu ya ushambuliaji na ukabaji ili tufanye vizuri zaidi katika mchezo ujao dhidi ya JKT Ruvu,” alisema Omog.

Kocha huyo aliyewahi kuinoa Azam FC kabla ya kutua Simba, aliongeza kuwa wanaendelea na juhudi za kukisuka kikosi hicho ili kiweze kukabiliana na timu yoyote ya Ligi Kuu.

“Tuna muda wa kutosha kujipanga, kesho tunaendelea na mazoezi huku tukijitahidi kwa nguvu zote kuiweka timu katika hali nzuri ya kupambana kwenye mechi inayofuata,” alisema Omog.

Akizungumzia hali ya afya ya beki wa timu hiyo, Hamad Juma, aliyepata ajali hivi karibuni, Omog alisema anaendelea kupata matibabu akiwa mapumzikoni mkoani Tanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles