24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyakazi Arsenal ajiuzulu kutokana na Wenger kutosajili

Wenger
Wenger

LONDON, ENGALND

BAADA ya klabu ya Arsenal kufanya vibaya katika michezo yake miwili ya mwanzo kwenye michuano ya Ligi Kuu England, mfanyakazi wa klabu hiyo ameamua kutangaza kujiuzulu kwa madai kwamba timu hiyo inafanya vibaya kwa kuwa haifanyi usajili wa maana.

Katika mchezo wa mwanzo, Arsenal ilikubali kichapo cha mabao 4-3 kwenye uwanja wa nyumbani wa Emirates, kabla ya kutoka suluhu dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Leicester City, matokeo hayo tayari yamewafanya mashabiki wa klabu hiyo kuanza kumtupia lawama kocha Arsene Wenger.

Kocha huyo hadi sasa amefanya usajili wa baadhi ya wachezaji kama vile, Takuma Asano ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Sanf Hiroshima na Rob Holding ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Bolton, hata hivyo mashabiki wa klabu hiyo wamempigia kelele ya kutakiwa kusajili ili timu iweze kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu.

Inasemekana klabu hiyo ina jumla ya wafanyakazi 600 ambao wameajiriwa, hivyo fedha nyingi zinatumika katika kulipa mishahara wafanyakazi hao na kushindwa kusajili wachezaji wazuri wanaoweza kutoa mchango mkubwa kwenye timu.

Wenger amedai kuwa ana pauni milioni 300 ambazo anaweza kuzifanyia kazi ya usajili, lakini watu wanatakiwa kukumbuka kwamba katika klabu hiyo kuna wafanyakazi 600 ambao wanatakiwa kuwajibika.

Kutokana na kauli hiyo ya Wenger, mfanyakazi mmoja wa klabu hiyo ambaye pia ni mwanachama, ametuma barua kwa uongozi wa klabu ya kutaka kujiuzulu kutokana na kauli ya kocha Wenger, mfanyakazi huyo amedai kuwa anaona bora ajiuzulu ili idadi ya wafanyakazi ipungue na klabu hiyo iwe na fedha za kutosha kwa ajili ya usajili.

Amedai kwamba anaumia sana kuona klabu hiyo ikishindwa kufanya vizuri kwa muda mrefu na alikuwa hajui kama tatizo ni fedha za usajili, hivyo amechukua maamuzi ya kujiuzulu huku akiwa anasubiri majibu hadi ifikapo Septemba 9 mwaka huu.

Kuondoka kwa mfanyakazi huyo sasa klabu hiyo itakuwa na jumla ya wafanyakazi 599. Usajili wa wachezaji katika kipindi hiki cha majira ya joto bado unaendelea hadi kufikia Agosti 31 mwaka huu, hivyo klabu hiyo bado ina nafasi ya kufanya usajili wa nguvu na kuwafurahisha mashabiki wao.

Japokuwa mashabiki wengi wamekuwa wakimzoea kocha huyo kufanya usajili katika siku za mwisho za kufungwa kwa dirisha hilo, lakini sasa wameanza kumchoka na wapo ambao wanatamani kocha huyo ajiuzulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles