33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Ombeni Gabriel aibuka na ‘You Are My God’

ARIZONA, MAREKANI

MWANAMUZIKI wa gospo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) anayeishi nchini Marekani, Ombeni Gabriel, amewaomba mashabiki waipokeee video yake mpya, You Are My God.

Akizungumza na MTANZANIA, Gabriel alisema katika wimbo huo wenye ujumbe wa kumshukuru na kumtukuza Mungu amemshirikisha mwimbaji kutoka Uganda, Victoire Popole.

“Nimeachia video hivi karibuni ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube, bado nahitaji sapoti ya wadau na wapenzi wa muziki kutoka hapa Marekani na huko Afrika na ninajua ujumbe uliopo ndani ya You Are My God unamhusu kila mtu anayetaka kumshukuru Mungu,” alisema Gabriel.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles