23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema yaridhia NEC kumzuia Lissu

 FARAJA MASINDE– DAR ES SALAAM

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo(Chadema), imeridhia adhabu iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumfungia siku saba mgombea wake wa urais, Tundu Lissu.

Hatua hiyo, inakuja baada ya chama hicho kueleza sasa, Lissu wake ataanza kufanya kazi za kijamii ambazo atapangiwa na chama hicho.

Lissu alifungiwa na kamati kutofanya kampeni kuanzia Oktoba 3 hadi 9, mwaka huu kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa na viongozi wa vyama na NRA na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa madai ya kutoa maneneo ya uchochezi yasiyothibitika.

Akizungumza Dar es Salaam na waandishi wa hahari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema pamoja na kuridhia uamuzi huo, wamemshauri Lissu asiendelee na mikutano ya kampeni.

Alisema tayari wamepokea hukumu kutoka tume ambayo ilijaribu kujenga dhana ya kuonyesha haikuhusika moja kwa moja na adhabu hiyo.

“Pamoja na yote hayo, huu uamuzi tunajua ni wa chama fulani kwa maelekezo ya Serikali na wagombea wao kwa kutumia vyama vingine, Chadema tunapinga hii, tumeeleza kitengo chatu cha sheria haraka na kwa hati ya dharura kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga uamuzi huu.

“Tunajua kesi inaweza isijibiwe kwa wakati, ni muhimu tukaweka kwenye kumbukumbu mambo ambayo tunafikiri ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na sheria zilizopo na kanuni zinatumika kwa makusudi kuminya demokrasia.

“Tumemshauri mgombea wetu asindelee na kampeni kipindi hiki ambacho tume ilizuia mikutano yake, napenda kuwambia viongozi wetu na wanachama wetu wa Tanzania,Lissu siyo tu mgombea urais wa chama chetu, huyu ni makamu mwenyekiti wa chama,”alisema.

Alisema chama hicho kina kazi kubwa za kufanya, zikiwamo za kisiasa na kijamii na Lissu hatakosa kazi za kufanya kwa muda wa siku saba.

“Chama kitampangia programu mahususi kama makamu mwenyekiti wa chama kufanya majukumu ya kijamii,kisiasa katika maeneo ambayo chama kitapanga.

“Kama dhamira ilikuwa ni kufunga ujumbe usifike, kutakuwa na ujumbe wa makamu mwenyekiti wa chama katika kufanya kazi za kijamii na za kisiasa, tunaishukuru tume vilevile kwani kama wao walifikiri wanatuziba,tuna uwezo wa kuzibua vilevile,hataendeleza mikutano ya kampeni, bali atafanya majukumu ya mahususi ya kisiasa na kijamii, hivyo huo ndiyo msimamo wetu kama chama,” alisema Mbowe.

Zanzibar 

Katika hatua nyingine, Mbowe alisema wamekubalina kumuunga mkoano mgombea urais wa Zanzibar wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Self Sharif Hamad.

“Kamati Kuu jana(juzi) tumeamua, tumeridhika na baadhi ya kauli mbalimbali za viongozi wa vya vyetu vya Chadema na ACT Wazalendo, baada ya kushauriana kwa kina na mgombea wetu wa Zanzibar, Said Issa Mohammed ambaye ndiye alikuwa ameteuliwa, tumeona ni sahihi kabisa kumuunga mkono Maalim Seif, tutamuunga mkono,mgombea wetu ameridhia kujitoa mwenyewe kwenye kinyang’anyiro hicho.

“Pia chama chetu kinatambua umuhimu wa kushirikiana kwenye nafasi mbalimbali ya ubunge, udiwani, makao makuu tuamue, tunaendelea kushirikisha maeneo mbalimbali katika kuon akuwa tukiweze kushirikiana kwenye maeoe mbalimbali tutapata wawakilisha bora zaidi Kamati Kuu imeagiza kamati mbalimbali kulifanyia kazi hilo kwenye sehemu mbalimbali,” alisema Mbowe.

Akizungumzia muungano kwa upande wa Tanzania Bara, Mbowe alisema kuwa milango iko wazi iwapo vyama vitaridhia kuungana na chama hicho kwenye mbio za urais.

Wagombea kuenguliwa

Katika hatua nyingine, chama hicho kilisema kinasikitishwa na namna ambavyo NEC imewaenguwa wagombea wake wakiwamo na madiwani 577 hatua aliyosema kuwa ni uonevu.

“Wagombea wetu wengi wamecheleweshwa kufanya kampeni awamo Boniface Jacob wa jimbo la Ubungo, na Same Magharibi, Gervas Mgonja aliyefungiwa kwa wiki mbili, lakini kama hiyo haitoshi wagombea wetu wa udiwani 577 wameenguliwa jambo ambalo limetusononesha.

“Jambo la ajabu zaidi ni kuwa hakuna hata mgombea mmoja wa CCM aliyeenguliwa, hatua hii ni sababu inayoleta machafuko kwani zaidi ya asilimia 50 ya muda wa kampeni umepita na bado kuna wagombea wetu hawajapata majibu ya rufaa, hivyo hata sisi kuna mambo tunayaona kabisa siyo sahihi na tumekuwa tukiikumbusha tume bila mafanikio,” alisema Mbowe na kuomba tume hiyonkutenda haki pande zote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles