24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Okwi apangua mipango ya Phiri

Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri
Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri

NA JENNIFER ULLEMBO

UJIO wa mshambuliaji, Emmanuel Okwi katika klabu ya Simba, umepangua mipango ya Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Phiri, ambaye amelazimika kupangua kikosi chake alichokipanga kupitia mechi ya kirafiki dhidi ya KMKM.

Okwi alijiunga katika kambi ya timu hiyo juzi visiwani Zanzibar, kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Habari za ndani kutoka katika kambi ya Simba, zilisema ujio wa mshambuliaji huyo umebadilisha mipango ya awali ya kikosi alichotaka kukisuka kocha Phiri hivyo ataanza upya.

Chanzo hicho kilisema kuwa mipango ya kocha huyo kwa sasa ni kupata ‘First Eleven’, baada ya mechi tatu za kirafiki.

“Kocha anamfahamu Okwi vizuri na amefurahi kusajiliwa kwake kwani anaamini mchezaji huyo ataongeza ushindani, lakini amelazimika kuanza kupanga upya kikosi chake cha kwanza,” kilisema chanzo hicho.

Mpashaji huyo alieleza kocha huyo amemsifu mshambuliaji huyo kwani licha ya kutofanya mazoezi kwa muda mrefu bado yupo fiti.

Timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles