26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisa wa Takukuru auawa kinyama

NA PENDO MANGALA, DODOMA

OFISA wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru)  Mkoa wa Dodoma, Emmanuel  Meta (37),  amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu baada ya kupigwa na watu ambao hawajafamika.

Akitoa taarifa ya kifo hicho kwa waandishi wa habari, Ofisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Mnyambuga kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, David Misime, alisema ofisa huyo wa Takukuru alipatwa na mkasa huo juzi saa 6.00 usiku kayika eneo la Area C.

“Mtoa taarifa wa awali wa tukio hilo ni Athuman Mtengwa ambaye pia ni mfanyakazi wa Takukuru mkazi wa Area D,  alisema alipigiwa simu na Emmanuel  ambaye ni mfanyakazi mwenzake pia ni rafiki yake wa karibu akimweleza kuwa anaomba msaada wa kupelekwa hospitali alikuwa amepigwa na wezi,” alisema David.

Kwa mujibu wa ofisa mnadhimu huyo,   rafiki yake huyo alidai kupigwa  wakati akirudi nyumbani kwake akitokea baa ya Rose Garden iliyopo Area C jirani na nyumbani kwake.

Alisema   wakati   Meta  akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alifariki dunia.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles