29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisa polisi mbaroni kwa tuhuma za rushwa ya Sh 30,000

Walter Mguluchuma, Katavi

ASKARI Polisi wawili wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi, wanashikiliwa kwa kumkamata mtu aliyefichua uhalifu wa mama aliyekukuwa akinyanyaswa na kumuomba rushwa ya Sh 30,000 ili wamwachie huru.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera, alisema askari hao ambao majina yao hakuyataja mmoja askari hao ana cheo cha mratibu msaidizi wa jeshi la polisi.

Alidai askari hao  wanadaiwa kumkamata kijana aliyempiga picha mama ambaye alifanyiwa ukatili wa kijinsia  kwa kufungwa minyororo shingoni na mkwe wake.

Homera alisema, mtu aliyeombwa rushwa na askari hao, alipiga picha mama huyo akifanyiwa vitendo hivyo na kisha kuzituma kwa baadhi ya viongozi wa mkoa huo.

 Alisema askari waliokamatwa wanadaiwa kutumiwa na mtu huyo aliyefanya ukatili huo  na kumkamata kijana huyo na kumtaka awapatie Sh 30,000.

Homera alidai kijana huyo alijitetea kuwa yeye ndie aliyemfichua mama huyo akifanyiwa ukatili, jambo ambalo askari hao hawakusikiliza na kuendelea kudai wapewe fedha ili wamwachie.

Alisema kijana huyo alitoa fedha hizo ili aachiwe huru na baada ya hapo alikwenda kulalamika kwa viongozi wa Polisi Mkoa wa Katavi ambao walichukua hatua ya kuwakamata na askari hao na kuwekwa mahabusu.

 Alisema kitendo alichofichua kijana huyo, kinaonyesha ndani ya mkoa huo bado kuna watu wanaofanyiwa ukatili wa kinjisia hivyo atahakikisha vitendo kama hivyo vinakomeshwa kaisa katika mkoa huo.

 Aliagiza jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi kuhakikisha linamsaka na kumfikisha mahakamani mtuhumiwa alinayedaiwa kumtesa mama mkwe wake.

 Pia alilipongeza jeshi hilo kwa hatua za kuwakamata askari hao na kuendelea kuwashikilia kwa uchunguzi zaidi.

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga alisema askari hao wote wawili bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Alisema mara baada ya uchunguzi kukamilika, watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa taratibu za jeshi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles