24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Nywele za John Lennon zauzwa milioni 70/-

john-lennonNEW YORK, MAREKANI

NYWELE za aliyekuwa msanii wa muziki na mwanzilishi wa kundi la ‘The Beatles’, John Lennon, aliyeaga dunia miaka 36 iliyopita, zimeuzwa dola 35,000, ambapo ni zaidi ya Sh milioni 70 za Tanzania.

Msanii huyo alifanya vizuri katika muziki miaka ya zamani, lakini baada ya kufa nywele zake zilihifadhiwa ambapo juzi zilipigwa mnada nchini Marekani.

Kinyozi wa mwimbaji huyo alificha nywele baada ya kumnyoa msanii huyo alipokuwa akijiandaa kuigiza moja ya filamu zake.

Lennon aliuawa kwa risasi mwaka wa 1980 mjini New York, nchini Marekani na watu wasiojulikana. Mnunuzi wa nywele hizo ni shabiki sugu wa Lennon kutoka nchini Uingereza.

Bidhaa nyingine zilizotumika na kundi hilo la muziki la ‘The Beatles’ pia ziliuzwa katika mnada huo huko Texas. Baadhi ya bidhaa hizo ilikuwa nakala maalumu ya albamu yao ya ‘Yesterday and Today’, iliyouzwa kwa dola 150,000, sawa na zaidi ya Sh milioni 300 za Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles