23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Bow Wow athibitisha kutoka na Keyshia Cole

Bow Wow na Keyshia ColeNEW YORK, MAREKANI

BAADA ya mkali wa muziki Shad Moss ‘Bow Wow’ kuachana na mpenzi wake wa zamani, Erica Mena, sasa msanii huyo ameweka wazi kwamba anatoka na mkali wa muziki wa RnB, Keyshia Cole.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, juzi Bow Wow aliweka picha akiwa na mrembo huyo na kusema kwamba ‘Kichwa kimepata sehemu ya kutulia’

Hata hivyo, rafiki wa karibu na Bow Wow alisema kwamba wawili hao kwa sasa wapo katika uhusiano, lakini mambo yao yanafanyika chini kwa chini.

Bow Wow kwenye akaunti yake ya Instagram aliandika kwamba uhusiano wake wa sasa ni bora zaidi ya mwaka jana, hivyo anaamini atadumu kwa muda mrefu na mpenzi mpya, japokuwa hakumtaja ni nani.

Msanii huyo alikuwa chini ya kundi la Young Money Cash Money, lakini mwaka jana aliamua kujitoa na kufanya kazi pamoja na Snoop Doggy, ambaye ndiye aligundua kipaji cha masanii huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles