26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Nyumba, vibanda 50 vyakumbwa na bomoabomoa

bomoa

LEONARD MANG’OHA Na FERDANANDA MBAMILA, DAR ES SALAAM

NYUMBA na vibanda vya biashara zaidi ya 50 vimevunjwa katika zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam, katika Kata ya Mbezi.

MTANZANIA lilishuhudia tingatinga lenye namba za usajili T 583 BSH likiendelea kuvunja nyumba na vibanda hivyo katika eneo hilo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi, huku wakazi na wafanyabiashara wakihaha kuokoa mali zao.

Kuvunjwa kwa nyumba hizo kunaelezwa ni kupisha ujenzi unaoendelea wa barabara itokayo Goba kuungana na barabara kuu ya Morogoro.

Baadhi ya wanawake walionekana wakiangua vilio huku wakilalamika kutopewa muda wa kutosha kuondoa vitu vyao hivyo hawajui wataenda wapi kupata hifadhi baada ya nyumba zao kuvunjwa.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Diwani wa Kata ya Mbezi, Humphrey Sambo, alisema baada ya kupokea barua ya kuvunjwa kwa nyumba hizo, alifuatilia suala hilo na kubaini kuwa wananchi hao wamekuwapo eneo hilo tangu miaka ya 1970.

“Hivi karibuni tukiwa katika Uchaguzi wa Meya wa Kibamba, Mkuu wa Wilaya alinihakikishia kuwa zoezi hilo halitakuwapo hadi pale wakazi wa eneo hilo watakapokuwa wamefidiwa.

“Lakini jambo la kushangaza ni kwamba jana wamekuja na kutoa tangazo la watu kuhamisha vitu vyao na kuanza kuvunja hata kabla ya wananchi hao hawajatoa mali zao,” alisema Sambo.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini, alisema wameishi katika eneo hilo tangu mwaka 1974 baada ya kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa kabla ya mwaka 2004 wakala wa barabara Tanroads kuweka vigingi na kuwataka wahame ndani ya siku saba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles