28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Marie Stopes kutoa huduma ya uzazi bure

Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes, Anil Tambay
Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes, Anil Tambay

Na HARRIETH MANDARI, DAR ES SALAAM

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kupata huduma ya uzazi wa mpango bure kuanzia Novemba 2-4, mwaka huu katika hospitali za Marie Stopes nchini.

Huduma hiyo inafanyika ikiwa ni maadhimisho ya miaka 40 ya Shirika la Kimataifa la Marie Stopes duniani.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes, Anil Tambay, alisema bado Watanzania wengi wana idadi kubwa ya watoto na hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuhakikisha wanapata elimu ya uzazi wa mpango.

Alisema wanawake wengi, hasa waishio vijijini, huzaa wastani wa watoto wanne hadi watano hali ambayo ni hatari kwa uchumi wa nchi.

“Mwaka jana Marie Stopes duniani ilitoa huduma kwa watu milioni 21 ambao  walikuwa wanatumia angalau njia mojawapo ya uzazi wa mpango, ikiwa ni sehemu ya watu milioni 291 ambao wanatumia huduma hiyo,” alisema.

Tambay alisema mimba za utotoni na zisizotarajiwa bado zinaongezeka, kwamba mwaka jana takribani asilimia 27 ya wasichana wadogo walianza kuzaa ikilinganishwa na asilimia 23 ya mwaka 2010.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya wa Marie Stopes, Joseph Kominihangiro, alisema shirika hilo pia lina mradi wa huduma ya uchunguzi ya kansa ya shingo ya uzazi  kwenye zahanati za shirika hilo nchini, ambayo imefanikiwa katika mikoa minane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles