Sharifa Mmasi, Mtanzania DigitalÂ
JUMLA ya wachezaji saba wa Kimataifa kutoka nchi tofauti, wanatarajiwa kushiriki mashindano ya wazi ya gofu ‘Tanzania Ladies Open’ yanayotarajia kuanza Oktoba 22-24, 2021 kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni Mercy Nyanchama na Mildred Malubi kutoka Kenya, Eva Magala wa Nigeria, Peace Kabasweka, Irene Nakalembe, Martha Babirye na Eva Magala wanaowakilisha Uganda.
Kwa upande wa Tanzania, ni Madina Iddi ambaye ametamba kuibuka kidedea katika mashindano hayo dhidi ya wapinzani wake.
“Nimejiandaa vema na niko fiti kuelekea Tanzania Ladies Open, mwaka huu Nitachukuwa ushindi kutokana na maandalizi niliyofanya,” ameeleza.