26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wimbo wa Burna Boy kuimbwa wakati wa kuapishwa kwa Biden

Washington, Marekani

Msanii wa Nigeria, Burna Boy amejumuishwa katika orodha ya miziki itakayochezwa wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa Rais mteule Joe Biden.

Nyimbo ya Burna kwa jina Destiny itakuwa miongoni mwa nyimbo za wasanii wengine wa kimataifa.

Orodha ya nyimbo hizo 46 zimeandaliwa katika sherehe ya kuapishwa kwa Biden, taarifa hiyo imesema.

“Wasanii na nyimbo zilizochaguliwa ujumuisha taswira ya kila mmoja Marekani. Wanafungua ukurasa mpya na watasaidia kuleta watu pamoja wakati utawala wa Biden na Harris unaanza kazi yake muhimu ya kuunganisha nchi yetu,” taarifa hiyo imesema.

Nyimbo nyingine zilizochaguliwa ni pamoja na wasanii wakubwa kama Beyoncé na nyimbo yake Find Your Way Back, Kendrick Lamar na Mary J. Blige‘s na wimbo wao Now Or Never, Bob Marley na Wailers na nyimbo yao Could You Be Loved pamoja na Levitating hit ya Dua Lipa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles