29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Nyaraka za Kaseja zaungua

Pg 29.feb 13NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Kazi Tanzania, Kitengo cha Usuluhishi na Uamuzi (CMA), jana imeipiga kalenda kesi inayomkabili aliyekuwa kipa wa Yanga SC, Juma Kaseja, hadi Machi 10 mwaka huu kutokana na nyaraka za upande wa walalamikiwa kuungua moto.

Kaseja alishtakiwa na timu yake hiyo ya zamani ikidai fidia ya Sh milioni 340, ambayo ni Sh milioni 40 pamoja na fidia ya Sh milioni 300, ambazo ni gharama za usumbufu wa kuvunja mkataba, kumhudumia na kutunza kiwango chake kwa kipindi chote alichokuwa Yanga.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa jana saa 5 asubuhi kwenye mahakama hiyo, kwa pande hizo mbili mbele ya Msuluhishi Fimbo, aliyesikiliza shauri hilo kwa niaba ya Masse aliyepata udhuru.

Kaseja alifika CMA na Mwanasheria, Mwenda Nestory, aliyemuwakilisha mwanasheria wake, Samson Mbamba, aliyepata udhuru, huku upande wa walalamikaji (Yanga) ukiwakilishwa na Mkuu wa Idara ya Sheria, Frank Chacha.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kusikilizwa shauri hilo, Chacha alisema shauri limeahirishwa baada yanyaraka za utetezi kwa upande wa walalamikiwa kuungua moto.

“Upande wa walalamikiwa umeomba kusogezwa mbele kwa shauri hilo, ilikuandaa utetezi wao, baada ya ofisi yao ya Mbamba & Company Advocate kuungua moto, hivyo nyaraka muhimu za kesi hiyo nazo kuteketea.

“Kutokana na hali halisi ya suala hilo, sisi upande wa walalamikaji tulikubaliana na ombi lao na hivyo tunasubiria Machi 10 kesi hiyo itakapoendelea tena kwa hatua ya usuluhishi baada ya walalamikiwa kuandaa upya nyaraka zao,” alisema.

Ofisi za Mbamba & Company Advocate zilikuwa ndani ya jengo la ghorofa tatu la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), lililopo Mtaa wa Moscow na Libya eneo la Posta, Dar es Salaam lililowaka moto juzi na baadhi ya vyumba kuteketea moto.

Wakati huohuo, Chacha aliliambia MTANZANIA kuwa, Jumatatu ijayo kesi nyingine inayomkabili mshambuliaji wao wa zamani, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ nayo itaanza kusikilizwa CMA.

Yanga ilimshtaki Jaja ikidai fidia ya dola za Marekani 154,000 (Shmilioni 267) kwa kuvunja mkataba wake isivyohalali, fidia hiyo ni ya gharama za kufundishwa dola 100,000 pamoja na dola 54,000 za mshahara wake kwa miezi 18 iliyokuwa imebakia kwenye mkataba wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles