31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NYAMA YA BAA NI HATARI KWA WALAJI – KITUO

Na BENJAMIN MASESE -MWANZA

KITUO cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Wanyama Kanda ya Ziwa( ZVIC) kimewataka Watanzania  kuondokana na tabia na mazoea ya kula nyama ambayo  haijathibitishwa na daktari wa mifugo.

Kaimu Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Subira Samweli,alisema yamekuwapo   mazoea ya watanzania ya kula nyama  ambayo haijapitia katika machinjio  yanayotambulika.

Alisema kitendo ambacho kinawafanya kula kitoweo ambacho hakijathibitishwa na daktari wa mifugo.

“Watu ambao wapo katika hatari ya kupata maradhi ni wale ambao mara nyingi wanapenda kula kwenye baa,  migahawa, harusi, gengeni na sehemu nyingine ambazo  mara nyingi hazizingatii usalama na afya kwa walaji.

“Tabia hii imejengeka kwa jamii yetu na wala hata hawahoji kama nyama wanayokula imekaguliwa.

“Leo hii baa nyingi zinajinchijia mbuzi katika maeneo yao, hivyo hivyo kwenye harusi, migahawa na magenge, wanyama hao wana magonjwa mbalimbali hivyo ni vema watu wakaepuka kula nyama ambayo hajapitia kwa mtalaamu,” alisema.

Aliwataka maofisa mifugo wa mikoa, wilaya, tarafa, kata , vijiji na mitaa kuwa na utaratibu wa kufanya operesheni katika maeneo yao  kukomesha vitendo vya watu kuchinja ovyo katika maeneo ya biashara zao bila kuthibitishwa na mtaalamu wa mifugo.

Akizungumzia takwimu za ng’ombe waliofikishwa katika mnada wa Nyamatala na kuuzwa kwa ajili ya kitoweo kati ya Novemba 2016 hadi sasa ni Juni 2017, alisema  mwitikio  wa wafanyabiashara umepungua.

“Ukiangalia  mnada ulipoanza Novemba 2016, ng’ombe waliofikishwa  sokoni ni 6,556 na waliouzwa na kupata vibali kwenda kuchinjwa ni 4698, lakini kwa kipindi  cha Juni mwaka huu ng’ombe waliofikishwa ni 11,139, cha kusikitishwa waliouzwa ni 3,716 pekee.

“Hapo utaona jinsi gani  kuna  idadi kubwa ya mifugo iliyopelekwa lakini iliyouzwa ni kidogo. Pale Nyamatala bado miundombinu ya mbuzi na kondoo inatenegenzwa ili nao wapelekwe na  si kuuzwa  tena  Igoma,”alisema.

Samweli   alishangazwa na kitendo cha halmashauri za mikoa hiyo kutokuwa na utaratibu wa kutuma takwimu za mifugo ikizingatiwa   kwa kipindi   cha Julai ni halmashauri 11 pekee zilizotuma ripoti zao.

Alizitaja halmashauri hizo kuwa ni Serengeti, Msalala, Bukoba, Ushetu, Musoma , Shinyanga mjini  na Vijini, Misenyi, Rorya, Bunda Mjini na Vijiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles