26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Nuru the Light: Wasanii msiige ya Nigeria

Nuru the lightNA JULIET MORI (TUDARCO)

MSANII wa Bongo Fleva anayefanyia shughuli zake za kimuziki nchini Sweden, Nuru Magram ‘Nuru the Light’ amewataka wasanii wa Tanzania waache kushindana na soko la sanaa la Nigeria kwa kuwa halifanani na soko la hapa.

Msanii huyo alisema hayo jana, alipotembelea ofisi za kampuni ya New Habari (2006) Ltd, inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, The African na Rai.

Alisema Wanigeria hawakuanza jana kuwekeza katika sanaa, ndiyo maana sanaa yao hubadilika kulingana na wakati, hivyo wasanii wa Tanzania hawatakiwi kuiga sanaa ya Nigeria kutokana na utofauti wa soko lake.

“Nigeria hubadilika badilika na walianza zamani, tunachotakiwa nasi tutengeneze soko la muziki wetu, kisha taratibu tutabadilika na kuwaiga wao, lakini si tufanyavyo sasa,’’ alisema Nuru, anayetaraji kutoka upya na wimbo aliouita ‘L’.

Alisema wimbo wa ‘L’ amewakilisha vitu vingi, ikiwemo ‘Light’, ‘love’, ‘life’ na vingine vingi vyenye uhai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles