26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Nuno atimuliwa, Conte kocha mpya Tottenham

LONDON, England

UONGOZI wa klabu ya Tottenham umemfungashia virago kocha wake raia wa Ureno, Nuno Espirito Santo, huku Antonio Conte akitarajiwa kuchukua mikoba yake.

Nuno mwenye umri wa miaka 47, aliajiriwa Juni, mwaka huu, na kusaini mkataba wa miaka miwili lakini mambo yamekuwa hovyo kwa kikosi chake, ambapo kinashika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England (EPL).

Taarifa zinadai kuwa tayari mabosi wa Tottenham wameshazungumza na Conte na Muitalia huyo amekubali ofa ya kuliongoza benchi la ufundi la timu hiyo kwa miezi 18.

Conte anayetarajiwa kuingia jijini London mapema wiki ijayo, kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Sky Sport, amekuwa nje ya kazi ya ukocha tangu alipobwaga manyanga Inter Milan mwishoni mwa msimu uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles