26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

North Mara: Mgodi hauhusiki na uchafuzi wa maji ya Mto Mara

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, umekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuhusu utiririshaji wa zebaki kwenye Mto Mara na kusema kuwa hauhusiki na uchafuzi huo.

Taarifa mgodi huo wa North Mara iliyotolewa leo Machi 11, imebainisha kuwa mbali na eneo husika kuwa umbali wa kilomita 80-85 chini ya mgodi, zebaki si sehemu ya orodha ya vitendanishi vya mgodi huo wala haitokei kiasili katika eneo hilo nakwamba, kama kuna zebaki yoyote iliyopatikana katika mto haiwezi kuhusishwa na mgodi.

“Tumepata taarifa za tuhuma zinayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utiririshaji wa zebaki kwenye Mto Mara, lakini umma unapswa kuelewa kuwa mgodi hauhusiki nan uchafuzi huo wa maji,” imeeleza taarifa ya mgodi huo.

Aidha, Meneja wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa, amesema Mamlaka ya Bonde la Maji ya Ziwa Viktoria mara kwa mara imekuwa ikichukua sampuli za maji katika maeneo yaliyo jirani na migodi na mgodi wenyewe una mpango madhubuti wa ufuatiliaji wa maji ya ardhini  na hakuna ushahidi wa kuwepo zebaki au uchafu mwingine wowote kwenye maji ndani au karibu na maeneo ya uzalishaji.

Amesema Serikali ya Tanzania iliunda timu ya wataalamu inayoongozwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ili kuhakikisha hakuna uchafuzi wa mazingira au maji unaotokea katika mgodi huo na katika maeneo yanayouzunguka.

“Mgodi pia umefikia lengo muhimu la uhifadhi wa taka zitokanazo a mchakato wa uchenjuaji wa madini kwa kupunguza kiasi cha maji yaliyohifadhiwa kwa kiasi kikubwa kutoka mita za ujazo milioni 7 hadi mita za ujazo 800,000 ndani ya kipindi cha miaka miwili, kama ilivyokubaliwa katika Mkataba wa Maelewano na NEMC.

“Haya ni mafanikio makubwa, ambayo yanaonyesha zaidi dhamira na jitihada za mgodi wa dhahabu wa North Mara zinakwenda sambamba kwa kuhakikisha hakuna uchafuzi wa maji au mazingira kwenye mgodi na maeneo yanayouzunguka,” amesema Mutagahywa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles