31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri nchini zapewa miezi mitatu kukabidhi vituo vya afya

*Ni vilivyojengwa kwa fedha za tozo

Na Safina Sarwatt, Mwanga

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI), David Silinde, amezitaka Halmashauri zote nchini ambazo zimepokea fedha za tozo kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya kuhakikisha kwamba wanaanza ujenzi huo kwa haraka na kuyakabidhi majengo hayo ifikapo Juni 30, mwaka huu.

Silinde ametoa maagizo hayo leo Ijumaa Machi 11,2022, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kirya ambapo alijionea ujenzi huo ukiendelea.

Amesema serikali kuu imetoa fedha za tozo kwa halmashauri 133 zilizopo hapa nchini ili ziweze kujenga Vituo vya afya ambapo kila halmashauri imepatiwa fedha kiasi cha Sh milioni 250 kwa ajili ya ujenzi huo.

“Serikali inataka kuona kasi ya ujenzi wa vituo vya afya, ambavyo vinatokana na fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan za tozo ambazo Rais Samia Suluhu Hassan, zinaendana na kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Uviko-19,” amesem Silinde.

Aidha, Naibu Waziri huyo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mwanga, Mwajuma Nasombe kwa usimamizi mzuri wa miradi ya serikali ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madara ya Uvico-19, huku akimtaka kasi hiyo pia iende kwenye ujenzi wa kituo cha afya Kirya.

Awali, akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kirya kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mkurugenzi mMtendaji wa Halmashauri hiyo Mwajuma Nasombe, amesema walipokea fedha kiasi cha Sh milioni 250 kutoka serikali kuu zikiwa ni fedha za tozo, ambapo mradi huo ulianza rasmi Februari 2022 ambapo mradi huo utakamilika Juni 30, mwaka huu.

Aidha, Nasombe ameiomba serikali kuleta fedha za nyongeza kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa majengo yaliyobaki ya chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto, wodi za wagonjwa, chumba cha kuhifadhi maiti ili kukamilisha majengo yote yanayohitajika kwa ngazi ya kituo cha afya.

Nae Diwani wa kata ya Kirya, Hassan Abbas, amesema kukamilika kwa mradi huo wa kituo cha afya Kirya, kutapunguza adha ya Wananchi kusafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 40 kufuata huduma za afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya na Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Jafari Kandege, wameahidi kuifuatilia miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles