31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Huduma za maji mtama zaimarika kwa zaidi ya asilimi 90

Na Hadija Omary, Lindi

Huduma  za upatikanaji wa maji safi na salama katika kata za Pangatena, Namangale na  Nyangamara Halmashauri ya mtama mkoani lindi zimeimarika kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo 2020-2022.

Hayo yamebainishwa na Afisa Miradi na Ufuatiliaji wa rasilimali za umma, inayofanywa katika miradi ya maji halmashauri hiyo ya Mtama, Karimu Mnedi alipokuwa akieleza mafanikio ya mradi huo katika kikao kilichofanyika katika kata ya Nyangao chenye lengo la kutoa mrejesho wa utekelezaji wa mradi huo .

Mradi huo wa kuimarisha uwezo wa ufuatiliaji wa rasilimali za umma kwa jamii katika  sekta ya maji  Halmashauri ya Mtama unatekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la RONDO WOMENS DEVELOPMENT ORGANIZATION (ROWODO) kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society(FCS).

Mnedi amesema uimarikaji huo umetokana na jitihada mbali mbali zilizofanya na shirika ilo ikiwa pamoja na kufanya ufuatiliaji wa ukarabati mkubwa wa miradi mitatu ya maji, mradi wa Namangale, Pangatena na Nyangamara na changamoto za uendeshaji wa miradi ya maji katika kata hizo.

Pia kuendeshamMafunzo juu ya usimamizi na utekelezaji wa pamoja wa sera na sheria Na. 5 ya Maji ya mwaka 2019 pamoja na ufuatiliaji wa rasilimali za umma ili kuwa na miradi endelevu pamoja na ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za mradi.

“Tumeweza kufikia malengo ya kuimarisha huduma za upatikanaji wa maji kwa sababu  wakati tunapokea mradi 2019 Mfano kwenye mradi wa maji ya Pangatena ambapo tangu kumalizika kwa shughuli za mkandarasi katika mradi huu uliogharimu Sh milioni 980, hali ya upatikanaji maji ilikuwa duni kiasi cha mradi kupewa sifa ya kuwa mradi kichefuchefu lakini kwa hivi sasa maji yanapatikana muda wote,” alifafanua Mnedi.

Hata hivyo, Mnedi alieleza hali ya upatikanaji wa maji kabla ya mradi na sasa ambapo katika kata ya pangatena imeongezeka kutoka asilimia 40 mwaka 2020 mpaka kufika asilimia 93, namangale kutoka asilimia 63 mwaka 2020 mpaka kufikia 95 mwaka 2022  huku nyangamara ikionezeka kwa asilimia 94 mwaka 2022 kutoka asilimia 78 mwaka 2020.

Nae Afisa kutoka Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA), Mhandisi Nasoro Mohamed, amesema kuwa  tangu shirika hilo la Rowodo lianze kushirikisha wananchi kulinda na kusimamia miradi yao  katika kata hizo mabadiliko makubwa yameanza kuonekana ikiwa pamoja na mapato yanayotokana na miradi hiyo kuongezeka, kupungua kwa migogoro na miradi kuwa endelevu.

“Sisi kama  Ruwasa sasa tunajivunia ROWODO kwa sababu uendelevu wa vituo vyetu vya maji kwa maeneo yenye mradi  umeongezeka kwani hapo awali unaweza kukuta kituo kimoja hakifanyi kazi kwa muda mrefu hata kwa miezi mitatu lakini kupitia mpango huu ile taarifa ya haraka tunaweza kuipata hivyo tunaishukuru Rowodo kwa ufuatiliaji wa karibu katika miradi hii na pia tunawaomba kama watakuwa na miradi mingine basi uwezo huu ujengwe hata katika kata zingine,” amesema Mhandisi Nasoro.

Akifunga kikao hiko muwakilishi wa katibu Tawala Wilaya ya Lindi, katibu tarafa halmashauri ya Mtama, Mudhihiri Njonjoro pamoja na kulipongeza shirika la ROWODO kwa kuwajengea uwezo wananchi wa kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma katika sekta hiyo ya maji lakini pia amesema jambo linalofanywa na shirika hilo ni diplomasia.

“Pamoja na wananchi wanadhani Diplomasia inahusisha mahusiano ya nchi na nchi lakini hata hili linalofanywa na Rowodo la kutatua migogoro na hata upatanishi kwa wananchi na jumuia za watumia maji ni moja ya kazi ya kidipromasia,” amesema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles