30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yazindua klabu nyingine ya uwezeshaji sekta ya madini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Benki ya NMB imeendeleza utaratibu wa kuwahudumia wadau wa sekta ya madini nchini kupitia mpango maalum wa kuwawezesha baada ya kuzindua jukwaa jingine kwa ajili hiyo kwenye mikoa ya kanda ya kaskazini.

Uzinduzi wa NMB Mining Club mpya ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha ambako maofisa waandamizi wa benki hiyo walisema lengo kuu la majukwaa hayo ni kusaidia ufanisi wa uwekezaji na maendeleo ya sekta ya madini nchini.

Taasisi hiyo ilianzisha utaratibuu huu rasmi mwezi Juni mwaka huu jijini Dodoma ambako uzinduzi wake rasmi ulifanywa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, baada ya wazo hili la kipekdee kuwa limetambulishwa mjini Kahama.

NMB Mining Club ya tatu ilianzishwa Mwanza mwezi ukiofuata ambako benki hiyo kubwa kuliko zote nchini ilisisitiza msimamo wake wa kuwakwamua wadau wa madini kifedha na kuwasaidia kufanya shughuli zao kisasa zaidi.

Kwa kuanzia, mpango huo unalenga kuifikia miji sita ambayo ni pamoja na Mwanza, Chunya, Morogoro, Arusha, Dodoma na Kahama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa la wadau wa madini wa Arusha juzi, Meneja was NMB wa Kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper, alisema uwekezaji huu umetokana na utafiti wa kutosha walioufanya kuhusu mahitaji ya wadau wa madini.

“Kinachofanyika leo ni baada ya kujiridhisha  kuwepo kwa mahitaji makubwa ya uwezeshaji kwa wananchi waliowekeza kwenye sekta hiyo hasa wa mitaji na vitendeakazi,” Prosper alisema.

Naye Meneja mwandamizi Kitengo cha Biashara wa NMB, Christopher Mgani, alisema katika kufanikisha hilo ipo mikopo tofauti ya kusaidia ukiwemo ule ambao ni kwa ajili ya kununulia vifaa vya uchimbaji.

Mgani alisema kuna unaohusu mteja kuchangia asilimia 30 ya gharama halisi ya  vifaa kama ni ambavyo vimetumika na asilimia 20 ya vifaa  vipya.

Wakati wa uzinduzi wa Dodoma Mining Club, NMB ilisema imejipanga kuwakopesha wadau wa madini takriban Sh bilioni 200 ifikapo mwaka 2025. Na hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu, mikopo ya madini ilikuwa zaidi ya Sh bilioni 63.

Miongoni mwa  wadau walioshiriki kwenye hafla hiyo ni pamoja na wachumbaji, wauzaji, na wanunuzi  wa  madini katika  mikoa ya kanda ya kaskazini ambao waliipongeza NMB kwa kuchangia maendeleo yao.

Wadau hao walisema mchango wa benki hiyo utakuwa wa manufaa makubwa kama swala la riba kubwa litatazamwa kwa namna tofauti. Katibu wa wachimbaji wadogo Mkoa wa Manyara, Rachel Njau, aliiomba NMB kusaidia kutoa elimu ya usimamizi wa fedha hasa mikopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles