24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yatoa milioni 25 kudhamini gofu ‘CDF Trophy’

NA WINFRIDA MTOI, MTANZANIA DIGITAL

BENKI ya NMB imetoa kiasi cha fedha sh. milioni 25 kudhamini mashindano ya gofu ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ‘CDF Trophy’ yanayotarajia kuanza Septemba 17-19 mwaka huu kwenye Viwanja vya Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi wa fedha hizo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum wa NMB, Getrude Mallya, amesema udhamini huo unatokana na ushirikiano wao na Klabu ya Gofu Lugalo, tangu  mwaka 2016 wamekuwa wadau wakubwa wa mchezo huo.

Getrude amesema pamoja na fedha hizo watagharamia vifaa mbalimbali kama vile fulana 200, kofia 200 na bendera 18 za kuweka kwenye viwanja ambavyo vina thamani ya milioni 35.

“Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Lugalo kwa kuendeleza michezo hasa gofu ambao umejizoelea mashabiki wengi.Tumekuwa wadau namba moja katika kuendeleza gofu, si hapa Lugalo bali na klabu nyinginea hadi Zanzibar,” amesema Getrude.

Akizungumzia mashindano hayo, Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, amesema yanafanyika kila mwaka ikiwa ni pamoja na kusherehekea  kuzaliwa kwa JWTZ.

Amesema mashindano yatahusisha klabu zote za gofu Tanzania na hadi sasa wachezaji zaidi ya 100 wamejisajili.

“Tumekaribisha  klabu zote kama vile Moshi Klabu, Arusha Gymkhana, Dar es Salaam na Morogoro Gymkhana, lakini pia  hata wale wachezaji binafsi,” amesema.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Gofu Tanzania, Injinia Boniface Nyiti, amesema shindano hilo ni kubwa na lipo katika kalenda ya chama hicho kila mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles