27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara yaijaza noti Taifa Stars

Juliana Samweli,TUDARCO

Waziri wa Habari Sanaa,Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa,  wizara yake imeizawadia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars fedha sh. Milioni 10 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar katika wa kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza leo Septemba 8, katika tamasha la utamaduni jijini Mwanza, Bashungwa amesema wametoa zawadi hiyo ili kuongeza hamasa kwa wachezaji.

“Mdau yeyote  anayetaka kutoa  zawadi  ya hamasa kwa  Taifa Stars, naomba iwasiliane na wizara ili kuitambua, hongereni sana Taifa Stars na Watanzania wote,” amesema Bashungwa.

Amesema katika kuendeleza sekta ya michezo nchini, amewaomba Watanzania kuendelea kuiunga mkono timu ya Taifa ili kufanya vizuri kwani Rais Samia Suluhu Hassani ameweka mazingira mazuri ya kukuza michezo.

 Aidha  ameeleza kuwa katika Mkoa wa Mwanza kuna mipango mizuri ya  kuboresha Uwanja wa CCM Kilumba ili jitihada za kufufua timu  ya Pamba ziendane na miundombinu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles