23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yatenga Mil 240 kwa washindi wa Promosheni ya MastaBata

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BENKI ya NMB imezindua msimu wa tatu wa Kampeni ya Kuhamasisha Matumizi ya Kadi na Masterpass QR iitwayo ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ ambako imetenga kiasi cha Sh milioni 240 zitakazo shindaniwa katika kipindi cha wiki 10.

Tofauti na misimu iliyopita ya ‘NMB MastaBata’ na ‘NMB MastaBata – Sio Kikawaida,’ iliyohusisha zawadi za bidhaa mbalimbali, kampeni hiyo msimu huu itatoa zawadi za pesa taslimu tu kwa wateja 1,080 – uamuzi unaolenga kumpa mteja uhuru wa kuchagua matumizi ya pesa atazoshinda.

Promosheni hiyo mpya inayojulikana kama NMB MastaBata, Kivyako Kivyako, ilianza rasmi siku ya ijumaa na itaendelea kwa muda wa wiki 10 mfululizo huku zawadi zikitolewa baada ya kila siku saba na kila mwezi.

Tangu mwaka 2018, NMB imekuwa ikiendesha kampeni za MastaBata kuchagiza matumizi ya kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR miongoni mwa wateja wake.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo kwenye makao makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo, Juma Kimori, alisema mara hii zawadi ni pesa taslimu tu ili kuwapa uhuru washindi kuzitumia wanavyotaka.

Washindi wa kila wiki watanyakua Sh 100,000 na milioni 1 kila mwezi. Kwenye droo ya mwisho, washindi 30 watashinda jumla ya Sh milioni 90.

“Ili kurudisha faida tunayoipata kama benki kwa wateja wetu, tumezindua promosheni hii itakayoshuhudia zawadi ya pesa taslimu zikitolewa kwa wateja wetu na pesa hii itawekwa katika akaunti zao ili kuwahamasisha waendelee kufanya malipo kwa kadi au Masterpass QR.

“Huu ni mwaka wa tatu wa kampeni za kuhamasisha matumizi ya kadi na Masterpass QR. Tulianza 2018 na MastaBata, tukaja na MastaBata – Siyo Kikawaida na leo kwa mwendelezo huo huo tunazindua MastaBata – KivyakoVyako tukimpa mshindi maamuzi ya kujichagulia cha kufanya na fedha atakayoshinda- yaani Bata la Kivyakovyako!,” amesema Kimori.

Mbali na kuhamasisha malipo ya kidijitali na kusaidia juhudi za kuifanya Tanzania kuwa uchumi usiotegemea sana pesa taslimu, pia NMB inaitumia kampeni hii kuwalipa fadhila wateja wake waaminifu.

Kimori alisema vile vile promosheni ya MastaBata – KivyakoVyako inatoa fursa kwa wateja wao kufurahia huduma za malipo ya kadi huku ikiwapa nafasi ya kushinda fedha zitakazofanya msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya kufana.

“Sisi kama NMB tunaedelea kuhamasisha matumizi ya kadi katika kufanya malipo mbalimbali hata kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia mitandao,” amebainisha.

Kwenye kampeni hii zawadi zitatolewa kwa washindi zaidi ya elfu moja ambao kati yao 100 watapatikana kila wiki, 25 kila mwezi na wale 30 wa kuhitimisha kampeni watanyakua 3m/- kila mmoja.

“Tofauti na mwaka jana, mwaka huu tumeamua kuwa na zawadi ya fedha tu ambazo zitawekwa kwenye akaunti za washindi. Lengo la benki ni kukuza manunuzi na malipo bila ya pesa taslimu- na ndio maana tumeona tuweke pesa hizi katika akaunti zao ili waendelee kuzitumia katika mifumo ile ile iliyowapa ushindi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles